1Bwana akamwambia Mose, 2“Sema na Waisraeli uwaambie: ‘Mimi ndimi Bwana Mungu wenu. 3Msifanye kama wafanyavyo huko Misri, mahali mlipokuwa mnaishi, wala msifanye kama wanavyofanya katika nchi ya Kanaani, mahali ninapowapeleka. Msifuate matendo yao. 4Ni lazima mzitii sheria zangu, na mwe waangalifu kuzifuata amri zangu. Mimi ndimi Bwana Mungu wenu. 5Zishikeni amri zangu na sheria zangu, kwa maana mtu anayezitii ataishi kwa hizo. Mimi ndimi Bwana. 6“‘Hakuna mtu awaye yote atakayemsogelea ndugu wa karibu ili kukutana naye kimwili. Mimi ndimi Bwana. 7“‘Usimvunjie heshima baba yako kwa kukutana kimwili na mama yako. Yeye ni mama yako; usiwe na mahusiano kama hayo naye. 8“‘Usikutane kimwili na mke wa baba yako; hiyo itamvunjia heshima baba yako. 9“‘Usikutane kimwili na dada yako, wala binti wa baba yako, au binti wa mama yako, awe amezaliwa katika nyumba hiyo au mahali pengine. 10“‘Usikutane kimwili na binti wa mwanao ama binti wa binti yako; utajivunjia heshima. 11“‘Usikutane kimwili na binti wa mke wa baba yako, aliyezaliwa na baba yako; huyo ni dada yako. 12“‘Usikutane kimwili na dada wa baba yako; ni ndugu wa karibu wa baba yako. 13“‘Usikutane kimwili na dada wa mama yako, kwa sababu ni ndugu wa mama yako wa karibu. 14“‘Usimvunjie heshima ndugu wa baba yako, kwa kukutana kimwili na mke wake; yeye ni shangazi yako. 15“‘Usikutane kimwili na mkwe wako, yeye ni mke wa mwanao; usiwe na mahusiano kama hayo naye. 16“‘Usikutane kimwili na mke wa kaka yako; utamvunjia heshima kaka yako. 17“‘Usikutane kimwili na mwanamke kisha na binti yake. Usikutane kimwili na binti wa mwanawe au binti wa binti yake; hao ni ndugu zake wa karibu. Huo ni uovu. 18“‘Usimchukue dada wa mke wako kuwa mke mwenza, na kukutana naye kimwili wakati bado mke wako anaishi. 19“‘Usimsogelee mwanamke ili kukutana naye kimwili wakati wa unajisi wa siku zake za mwezi. 20“‘Usikutane kimwili na mke wa jirani yako na kujitia naye unajisi. 21“‘Usimtoe mtoto wako yeyote awe kafara kwa mungu Moleki, kwani hutalinajisi kamwe jina la Mungu wako. Mimi ndimi Bwana. 22“‘Usikutane kimwili na mwanaume kama mtu akutanaye na mwanamke; hilo ni chukizo. 23“‘Usikutane kimwili na mnyama na kujitia unajisi kwake. Mwanamke asijipeleke kwa mnyama ili kukutana naye kimwili; huo ni upotovu. 24“‘Msijitie unajisi kwa njia yoyote katika hizi, kwa sababu hivi ndivyo mataifa nitakayoyafukuza mbele yenu yalivyojitia unajisi. 25Hata nchi ilitiwa unajisi, hivyo nikaiadhibu kwa dhambi zake, nayo nchi ikawatapika wakazi wake. 26Lakini ni lazima uzitunze amri zangu na sheria zangu. Mzawa na wageni waishio miongoni mwenu kamwe wasifanye mambo yoyote ya machukizo haya, 27kwa kuwa mambo haya yote yalifanywa na watu walioishi katika nchi hii kabla yenu, na nchi ikawa najisi. 28Kama mkiinajisi nchi, itawatapika kama ilivyowatapika mataifa yaliyowatangulia. 29“‘Kila mtu atakayefanya mojawapo ya machukizo haya, watu hao ni lazima wakatiliwe mbali na watu wao. 30Shikeni maagizo yangu, wala msifuate desturi za machukizo yoyote yaliyofanywa kabla hamjafika katika nchi hii, na kujitia unajisi kwa hayo. Mimi ndimi Bwana Mungu wako.’”
1Yahweh said to Moses, 2“Speak to the children of Israel, and say to them, ‘I am Yahweh your God. 3You shall not do as they do in the land of Egypt, where you lived: and you shall not do as they do in the land of Canaan, where I am bringing you; neither shall you walk in their statutes. 4You shall do my ordinances, and you shall keep my statutes, and walk in them: I am Yahweh your God. 5You shall therefore keep my statutes and my ordinances; which if a man does, he shall live in them. I am Yahweh. 6“‘None of you shall approach anyone who are his close relatives, to uncover their nakedness: I am Yahweh. 7“‘You shall not uncover the nakedness of your father, nor the nakedness of your mother: she is your mother. You shall not uncover her nakedness. 8“‘You shall not uncover the nakedness of your father’s wife. It is your father’s nakedness. 9“‘You shall not uncover the nakedness of your sister, the daughter of your father, or the daughter of your mother, whether born at home, or born abroad. 10“‘You shall not uncover the nakedness of your son’s daughter, or of your daughter’s daughter, even their nakedness: for theirs is your own nakedness. 11“‘You shall not uncover the nakedness of your father’s wife’s daughter, conceived by your father, since she is your sister. 12“‘You shall not uncover the nakedness of your father’s sister: she is your father’s near kinswoman. 13“‘You shall not uncover the nakedness of your mother’s sister: for she is your mother’s near kinswoman. 14“‘You shall not uncover the nakedness of your father’s brother, you shall not approach his wife. She is your aunt. 15“‘You shall not uncover the nakedness of your daughter-in-law: she is your son’s wife. You shall not uncover her nakedness. 16“‘You shall not uncover the nakedness of your brother’s wife. It is your brother’s nakedness. 17“‘You shall not uncover the nakedness of a woman and her daughter. You shall not take her son’s daughter, or her daughter’s daughter, to uncover her nakedness; they are near kinswomen: it is wickedness. 18“‘You shall not take a wife to her sister, to be a rival, to uncover her nakedness, while her sister is yet alive. 19“‘You shall not approach a woman to uncover her nakedness, as long as she is impure by her uncleanness. 20“‘You shall not lie carnally with your neighbor’s wife, and defile yourself with her. 21“‘You shall not give any of your children to sacrifice to Molech; neither shall you profane the name of your God. I am Yahweh. 22“‘You shall not lie with a man, as with a woman. That is detestable. 23“‘You shall not lie with any animal to defile yourself with it; neither shall any woman give herself to an animal, to lie down with it: it is a perversion. 24“‘Don’t defile yourselves in any of these things: for in all these the nations which I am casting out before you were defiled. 25The land was defiled: therefore I punished its iniquity, and the land vomited out her inhabitants. 26You therefore shall keep my statutes and my ordinances, and shall not do any of these abominations; neither the native-born, nor the stranger who lives as a foreigner among you; 27(for all these abominations have the men of the land done, that were before you, and the land became defiled); 28that the land not vomit you out also, when you defile it, as it vomited out the nation that was before you. 29“‘For whoever shall do any of these abominations, even the souls that do them shall be cut off from among their people. 30Therefore you shall keep my requirements, that you do not practice any of these abominable customs, which were practiced before you, and that you do not defile yourselves with them. I am Yahweh your God.’”
1Verder sprak de HEERE tot Mozes, zeggende: 2Spreek tot de kinderen Israels en zeg tot hen: Ik ben de HEERE, uw God! 3Gij zult niet doen naar de werken des Egyptischen lands, waarin gij gewoond hebt; en naar de werken des lands Kanaan, waarheen Ik u brenge, zult gij niet doen, en zult in hun inzettingen niet wandelen. 4Mijn rechten zult gij doen, en Mijn inzettingen zult gij houden, om in die te wandelen; Ik ben de HEERE, uw God! 5Ja, Mijn inzettingen en Mijn rechten zult gij houden; welk mens dezelve zal doen, die zal door dezelve leven; Ik ben de HEERE! 6Niemand zal tot enige nabestaande zijns vleses naderen, om de schaamte te ontdekken; Ik ben de HEERE! 7Gij zult de schaamte uws vaders en de schaamte uwer moeder niet ontdekken; zij is uw moeder; gij zult haar schaamte niet ontdekken. 8Gij zult de schaamte der huisvrouw uws vaders niet ontdekken; het is de schaamte uws vaders. 9De schaamte uwer zuster, der dochter uws vaders, of der dochter uwer moeder, te huis geboren of buiten geboren, haar schaamte zult gij niet ontdekken. 10De schaamte der dochter uws zoons, of der dochter uwer dochter, haar schaamte zult gij niet ontdekken; want zij zijn uw schaamte. 11De schaamte van de dochter der huisvrouw uws vaders, die uw vader geboren is (zij is uw zuster), haar schaamte zult gij niet ontdekken. 12Gij zult de schaamte van de zuster uws vaders niet ontdekken; zij is uws vaders nabestaande. 13Gij zult de schaamte van de zuster uwer moeder niet ontdekken; want zij is uwer moeder nabestaande. 14Gij zult de schaamte van den broeder uws vaders niet ontdekken; tot zijn huisvrouw zult gij niet naderen; zij is uw moei. 15Gij zult de schaamte uwer schoondochter niet ontdekken; zij is uws zoons huisvrouw; gij zult haar schaamte niet ontdekken. 16Gij zult de schaamte der huisvrouw uws broeders niet ontdekken; het is de schaamte uws broeders. 17Gij zult de schaamte ener vrouw en harer dochter niet ontdekken; de dochter haars zoons, noch de dochter van haar dochter zult gij nemen, om haar schaamte te ontdekken; zij zijn nabestaanden; het is een schandelijke daad. 18Gij zult ook geen vrouw tot haar zuster nemen, om haar te benauwen, mits haar schaamte nevens haar, in haar leven, te ontdekken. 19Ook zult gij tot de vrouw in de afzondering van haar onreinigheid niet naderen, om haar schaamte te ontdekken. 20En gij zult niet liggen bij uws naasten huisvrouw ter bezading, om met haar onrein te worden. 21En van uw zaad zult gij niet geven, om voor den Molech door het vuur te doen gaan; en den Naam uws Gods zult gij niet ontheiligen; Ik ben de HEERE! 22Bij een manspersoon zult gij niet liggen met vrouwelijke bijligging; dit is een gruwel. 23Insgelijks zult gij bij geen beest liggen, om daarmede onrein te worden; een vrouw zal ook niet staan voor een beest, om daarmede te doen te hebben; het is een gruwelijke vermenging. 24Verontreinigt u niet met enige van deze; want de heidenen, die Ik van uw aangezicht uitwerpe, zijn met alle deze verontreinigd; 25Zodat het land onrein is, en Ik over hetzelve zijn ongerechtigheid bezoeke, en het land zijn inwoners uitspuwt. 26Maar gij zult Mijn inzettingen en Mijn rechten onderhouden, en van al die gruwelen niets doen, inboorling noch vreemdeling, die in het midden van u als vreemdeling verkeert. 27Want de lieden dezes lands, die voor u geweest zijn, hebben al deze gruwelen gedaan; en het land is onrein geworden. 28Dat u dat land niet uitspuwe, als gij hetzelve zult verontreinigd hebben; gelijk als het het volk, dat voor u was, uitgespuwd heeft. 29Want al wie enige van deze gruwelen doen zal, die zielen, die ze doen, zullen uit het midden van haar volk uitgeroeid worden. 30Daarom zult gij Mijn bevel onderhouden, dat gij niet doet van die gruwelijke inzettingen, die voor u zijn gedaan geweest, en u daarmede niet verontreinigt; Ik ben de HEERE, uw God!
Bonyeza Enter ili kuuwekea mstari huu rangi, kuandika maelezo au kuunakili. Vitufe vya mishale vinakupeleka kwenye mstari unaofuata.
Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.