1Hii ndiyo migawanyo ya mabawabu: Kutoka kwa wana wa Kora alikuwa: Meshelemia mwana wa Kore, mmoja wa wana wa Asafu. 2Meshelemia alikuwa na wana wafuatao: Zekaria mzaliwa wa kwanza, Yediaeli wa pili, Zebadia wa tatu, Yathnieli wa nne, 3Elamu wa tano Yehohanani wa sita na Eliehoenai wa saba. 4Obed-Edomu naye alikuwa na wana wafuatao: Shemaya mzaliwa wa kwanza, Yehozabadi wa pili, Yoa wa tatu, Sakari wa nne, Nethaneli wa tano, 5Amieli wa sita, Isakari wa saba, na Peulethai wa nane. (Kwa kuwa Mungu alikuwa amembariki Obed-Edomu.) 6Shemaya mwanawe pia alikuwa na wana, waliokuwa viongozi katika jamaa ya baba yao kwa sababu walikuwa watu wenye uwezo mkubwa. 7Wana wa Shemaya ni: Othni, Refaeli, Obedi na Elizabadi; jamaa zake Elihu na Semakia walikuwa pia watu wenye uwezo. 8Hawa wote walikuwa wazao wa Obed-Edomu; wao na wana wao na jamaa zao walikuwa watu wenye uwezo pamoja na nguvu za kufanya kazi. Wazao wa Obed-Edomu jumla yao walikuwa sitini na wawili. 9Meshelemia alikuwa na wana na jamaa zake, waliokuwa watu wenye uwezo: jumla yao watu kumi na wanane. 10Hosa, Mmerari, alikuwa na wana wafuatao: Shimri alikuwa mkuu wao (baba yake alikuwa amemweka yeye kuwa mkuu ijapokuwa hakuwa mzaliwa wa kwanza), 11Hilkia wa pili, Tabalia wa tatu na Zekaria wa nne. Wana na jamaa za Hosa jumla yao walikuwa watu kumi na watatu. 12Hii migawanyo ya mabawabu, kupitia wakuu wao, walikuwa na zamu za kuhudumu hekaluni mwa Bwana kama jamaa zao walivyokuwa nazo. 13Kura zilipigwa kwa kila lango, kufuatana na jamaa zao, wakubwa kwa wadogo. 14Kura ya Lango la Mashariki ilimwangukia Shelemia. Kisha wakapiga kura kwa Zekaria mwanawe, aliyekuwa mshauri mwenye hekima, nayo kura ya Lango la Kaskazini ikamwangukia. 15Kura ya Lango la Kusini ikamwangukia Obed-Edomu, nayo kura ya maghala ikawaangukia wanawe. 16Kura za Lango la Magharibi na Lango la Shalekethi kwenye barabara ya juu zikawaangukia Shupimu na Hosa. Zamu za walinzi ziligawanywa kwa usawa: 17Kulikuwa na Walawi sita kila siku upande wa mashariki, wanne upande wa kaskazini, wanne upande wa kusini, na wawili wawili kwa mara moja kwenye ghala. 18Kuhusu ukumbi kuelekea magharibi, kulikuwa na wanne barabarani na wawili kwenye ukumbi wenyewe. 19Hii ndiyo iliyokuwa migawanyo ya mabawabu waliokuwa wazao wa Kora na wa Merari. 20Katika Walawi, Ahiya alikuwa mwangalizi wa hazina za nyumba ya Mungu na mwangalizi wa hazina za vitu vilivyowekwa wakfu. 21Wazao wa Ladani, waliokuwa Wagershoni kupitia Ladani na waliokuwa viongozi wa jamaa za Ladani Mgershoni, walikuwa Yehieli, 22wana wa Yehieli, wana wa Zethamu na wa nduguye Yoeli. Wao walikuwa waangalizi wa hazina za Hekalu la Bwana. 23Kutoka kwa wana wa Amramu, wana wa Ishari, wana wa Hebroni na wana wa Uzieli: 24Shebueli, mzao wa Gershomu mwana wa Mose, alikuwa afisa mwangalizi wa hazina. 25Jamaa zake kutoka kwa Eliezeri, wanawe walikuwa: Rehabia, Yeshaya, Yoramu, Zikri na Shelomithi. 26Shelomithi na jamaa zake walikuwa waangalizi wa hazina zote za vitu vile vilivyowekwa wakfu na Mfalme Daudi, kwa viongozi wa jamaa waliokuwa majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia, na kwa maafisa wengine wa jeshi. 27Baadhi ya nyara zilizotekwa vitani waliziweka wakfu kwa ajili ya ukarabati wa Hekalu la Bwana. 28Kila kitu kilichokuwa kimewekwa wakfu na Samweli mwonaji, na Sauli mwana wa Kishi, Abneri mwana wa Neri, na Yoabu mwana wa Seruya, pamoja na vitu vingine vyote vilivyokuwa vimewekwa wakfu, vyote vilikuwa chini ya uangalizi wa Shelomithi na jamaa zake. 29Kutoka kwa wana wa Ishari: Kenania na wanawe walipewa kazi nje ya Hekalu kama maafisa na waamuzi juu ya Israeli. 30Kutoka kwa wana wa Hebroni: Hashabia na jamaa zake, watu 1,700 wenye uwezo, waliwajibika katika Israeli magharibi ya Yordani kwa ajili ya kazi zote za Bwana na utumishi wa mfalme. 31Kuhusu wana wa Hebroni, Yeria alikuwa mkuu wao kufuatana na orodha ya jamaa yao. Katika mwaka wa arobaini wa utawala wa Daudi uchunguzi ulifanyika katika kumbukumbu, nao watu wenye uwezo miongoni mwa wana wa Hebroni wakapatikana huko Yazeri katika Gileadi. 32Yeria alikuwa na jamaa ya watu 2,700 waliokuwa watu wenye uwezo na viongozi wa jamaa, naye Mfalme Daudi akawaweka kuangalia Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila Manase kuhusu kila jambo lililomhusu Mungu na shughuli za mfalme.
1For the divisions of the doorkeepers: of the Korahites, Meshelemiah the son of Kore, of the sons of Asaph. 2Meshelemiah had sons: Zechariah the firstborn, Jediael the second, Zebadiah the third, Jathniel the fourth, 3Elam the fifth, Jehohanan the sixth, Eliehoenai the seventh. 4Obed-Edom had sons: Shemaiah the firstborn, Jehozabad the second, Joah the third, and Sacar the fourth, and Nethanel the fifth, 5Ammiel the sixth, Issachar the seventh, Peullethai the eighth; for God blessed him. 6Also to Shemaiah his son were sons born, who ruled over the house of their father; for they were mighty men of valor. 7The sons of Shemaiah: Othni, and Rephael, and Obed, Elzabad, whose brothers were valiant men, Elihu, and Semachiah. 8All these were of the sons of Obed-Edom: they and their sons and their brothers, able men in strength for the service; sixty-two of Obed-Edom. 9Meshelemiah had sons and brothers, valiant men, eighteen. 10Also Hosah, of the children of Merari, had sons: Shimri the chief, (for though he was not the firstborn, yet his father made him chief), 11Hilkiah the second, Tebaliah the third, Zechariah the fourth: all the sons and brothers of Hosah were thirteen. 12Of these were the divisions of the doorkeepers, even of the chief men, having offices like their brothers, to minister in Yahweh’s house. 13They cast lots, the small as well as the great, according to their fathers’ houses, for every gate. 14The lot eastward fell to Shelemiah. Then for Zechariah his son, a wise counselor, they cast lots; and his lot came out northward. 15To Obed-Edom southward; and to his sons the storehouse. 16To Shuppim and Hosah westward, by the gate of Shallecheth, at the causeway that goes up, watch against watch. 17Eastward were six Levites, northward four a day, southward four a day, and for the storehouse two and two. 18For Parbar westward, four at the causeway, and two at Parbar. 19These were the divisions of the doorkeepers; of the sons of the Korahites, and of the sons of Merari. 20Of the Levites, Ahijah was over the treasures of God’s house, and over the treasures of the dedicated things. 21The sons of Ladan, the sons of the Gershonites belonging to Ladan, the heads of the fathers’ households belonging to Ladan the Gershonite: Jehieli. 22The sons of Jehieli: Zetham, and Joel his brother, over the treasures of Yahweh’s house. 23Of the Amramites, of the Izharites, of the Hebronites, of the Uzzielites: 24and Shebuel the son of Gershom, the son of Moses, was ruler over the treasures. 25His brothers: of Eliezer, Rehabiah his son, and Jeshaiah his son, and Joram his son, and Zichri his son, and Shelomoth his son. 26This Shelomoth and his brothers were over all the treasures of the dedicated things, which David the king, and the heads of the fathers’ households, the captains over thousands and hundreds, and the captains of the army, had dedicated. 27They dedicated some of the plunder won in battles to repair Yahweh’s house. 28All that Samuel the seer, and Saul the son of Kish, and Abner the son of Ner, and Joab the son of Zeruiah, had dedicated, whoever had dedicated anything, it was under the hand of Shelomoth, and of his brothers. 29Of the Izharites, Chenaniah and his sons were for the outward business over Israel, for officers and judges. 30Of the Hebronites, Hashabiah and his brothers, men of valor, one thousand seven hundred, had the oversight of Israel beyond the Jordan westward, for all the business of Yahweh, and for the service of the king. 31Of the Hebronites was Jerijah the chief, even of the Hebronites, according to their generations by fathers’ households. In the fortieth year of the reign of David they were sought for, and there were found among them mighty men of valor at Jazer of Gilead. 32His brothers, men of valor, were two thousand seven hundred, heads of fathers’ households, whom king David made overseers over the Reubenites, and the Gadites, and the half-tribe of the Manassites, for every matter pertaining to God, and for the affairs of the king.
1Aangaande de verdelingen der poortiers: van de Korahieten was Meselemja, de zoon van Kore, van de kinderen van Asaf. 2Meselemja nu had kinderen; Zecharja was de eerstgeborene, Jediael de tweede, Zebadja de derde, Jathniel de vierde, 3Elam de vijfde, Johanan de zesde, Eljoenai de zevende. 4Obed-Edom had ook kinderen: Semaja was de eerstgeborene, Jozabad de tweede, Joah de derde, en Sachar de vierde, en Nethaneel de vijfde. 5Ammiel de zesde, Issaschar de zevende, Peullethai de achtste; want God had hem gezegend. 6Ook werden zijn zoon Semaja kinderen geboren, heersende over het huis huns vaders; want zij waren kloeke helden. 7De kinderen van Semaja waren Othni, en Refael, en Obed, en Elzabad, zijn broeders, kloeke lieden; Elihu, en Semachja. 8Deze allen waren uit de kinderen van Obed-Edom; zij, en hun kinderen, en hun broeders, kloeke mannen in kracht tot den dienst; daar waren er twee en zestig van Obed-Edom. 9Meselemja nu had kinderen en broeders, kloeke lieden, achttien. 10En Hosa, uit de kinderen van Merari, had zonen; Simri was het hoofd; (alhoewel hij de eerstgeborene niet was, nochtans stelde hem zijn vader tot een hoofd). 11Hilkia was de tweede, Tebalja de derde, Zecharja de vierde; al de kinderen en broederen van Hosa waren dertien. 12Uit dezen waren de verdelingen der poortiers onder de hoofden der mannen, tot de wachten tegen hun broederen, om te dienen in het huis des HEEREN. 13En zij wierpen de loten, zo de kleinen als de groten, naar hun vaderlijke huizen, tot elke poort. 14Het lot nu tegen het oosten viel op Salemja; maar voor zijn zoon Zecharja, die een verstandig raadsman was, wierp men de loten, en zijn lot is uitgekomen tegen het noorden; 15Obed-Edom tegen het zuiden; en voor zijn kinderen het huis der schatkameren. 16Suppim en Hosa tegen het westen, met de poort Schallechet, bij den opgaanden hogen weg, wacht tegenover wacht. 17Tegen het oosten waren zes Levieten; tegen het noorden des daags vier; tegen het zuiden des daags vier; maar bij de schatkameren twee en twee. 18Aan Parbar tegen het westen waren er vier bij den hogen weg, twee bij Parbar. 19Dit zijn de verdelingen der poortiers van de kinderen der Korahieten, en der kinderen van Merari. 20Ook was, van de Levieten, Ahia over de schatten van het huis Gods, en over de schatten der geheiligde dingen. 21Van de kinderen van Ladan, kinderen van den Gersonieten Ladan; van Ladan, den Gersoniet, waren hoofden der vaderen Jehieli. 22De kinderen van Jehieli waren Zetham en Joel, zijn broeder; dezen waren over de schatten van het huis des HEEREN. 23Voor de Amramieten, van de Jizharieten, van de Hebronieten, van de Uzzielieten, 24En Sebuel, de zoon van Gersom, den zoon van Mozes, was overste over de schatten. 25Maar zijn broeders van Eliezer waren dezen: Rehabja was zijn zoon, en Jesaja zijn zoon, en Joram zijn zoon, en Zichri zijn zoon, en Selomith zijn zoon. 26Deze Selomith en zijn broederen waren over al de schatten der heilige dingen, die de koning David geheiligd had, mitsgaders de hoofden der vaderen, de oversten over duizenden en honderden, en de oversten des heirs; 27Van de krijgen en van den buit hadden zij het geheiligd, om het huis des HEEREN te onderhouden. 28Ook alles, wat Samuel, de ziener, geheiligd had, en Saul, de zoon van Kis, en Abner, de zoon van Ner, en Joab, de zoon van Zeruja; al wat iemand geheiligd had, was onder de hand van Selomith en zijn broederen. 29Van de Jizharieten waren Chenanja en zijn zonen tot het buitenwerk in Israel, tot ambtlieden en tot rechters. 30Van de Hebronieten was Hasabja, en zijn broeders, kloeke mannen, duizend en zevenhonderd, over de ambten van Israel op deze zijde van de Jordaan tegen het westen, over al het werk des HEEREN, en tot den dienst des konings. 31Van de Hebronieten was Jeria het hoofd, van de Hebronieten zijner geslachten onder de vaderen; in het veertigste jaar des koninkrijks van David zijn er gezocht en onder hen gevonden kloeke helden in Jaezer in Gilead. 32En zijn broeders waren kloeke lieden, twee duizend en zevenhonderd hoofden der vaderen; en de koning David stelde hen over de Rubenieten, en Gadieten, en den halven stam der Manassieten, tot alle zaken Gods en de zaken des konings.
Bonyeza Enter ili kuuwekea mstari huu rangi, kuandika maelezo au kuunakili. Vitufe vya mishale vinakupeleka kwenye mstari unaofuata.
Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.