1Wakati huu Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, iitwayo Pasaka, ilikuwa imekaribia. 2Viongozi wa makuhani na walimu wa sheria walikuwa wanatafuta njia ya kumuua Yesu, kwa sababu waliwaogopa watu. 3Shetani akamwingia Yuda, aliyeitwa Iskariote, mmoja wa wale Kumi na Wawili. 4Yuda akaenda kwa viongozi wa makuhani na kwa maafisa wa walinzi wa Hekalu, akazungumza nao jinsi ambavyo angeweza kumsaliti Yesu. 5Wakafurahi na wakakubaliana kumpa fedha. 6Naye akakubali, akaanza kutafuta wakati uliofaa wa kumsaliti Yesu kwao, wakati ambapo hakuna umati wa watu. 7Basi ikawadia siku ya Mikate Isiyotiwa Chachu, siku ambayo mwana-kondoo wa Pasaka huchinjwa. 8Hivyo Yesu akawatuma Petro na Yohana, akisema, “Nendeni mkatuandalie chakula cha Pasaka ili tuweze kuila.” 9Wakamuuliza, “Unataka tukuandalie wapi?” 10Yesu akawaambia, “Tazameni, mtakapokuwa mkiingia mjini, mtakutana na mwanaume amebeba mtungi wa maji. Mfuateni mpaka kwenye nyumba atakayoingia. 11Nanyi mwambieni mwenye nyumba, ‘Mwalimu anauliza: Kiko wapi chumba cha wageni, ambamo mimi na wanafunzi wangu tutakula Pasaka?’ 12Atawaonyesha chumba kikubwa ghorofani, kikiwa kimepambwa vizuri. Andaeni humo.” 13Wakaenda, nao wakakuta kila kitu kama Yesu alivyowaambia. Hivyo wakaiandaa Pasaka. 14Wakati ulipowadia, Yesu akaketi mezani pamoja na wale mitume wake. 15Kisha akawaambia, “Nimetamani sana kuila Pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu. 16Kwa maana, nawaambia, sitaila tena Pasaka mpaka itakapotimizwa katika Ufalme wa Mungu.” 17Akiisha kukichukua kikombe, akashukuru, akasema, “Chukueni hiki mnywe wote. 18Kwa maana nawaambia tangu sasa sitakunywa tena katika uzao wa mzabibu, hadi Ufalme wa Mungu utakapokuja.” 19Kisha akachukua mkate, akashukuru, akaumega, na kuwapa, akisema, “Huu ni mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.” 20Vivyo hivyo baada ya kula, akakitwaa kikombe, akisema, “Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, imwagikayo kwa ajili yenu. 21Lakini mkono wake huyo atakayenisaliti uko hapa mezani pamoja nami. 22Mwana wa Adamu anaenda zake kama ilivyokusudiwa. Lakini ole wake mtu huyo amsalitiye.” 23Wakaanza kuulizana wenyewe ni nani miongoni mwao angeweza kufanya jambo hilo. 24Pia yakazuka mabishano katikati ya wanafunzi kwamba ni nani aliyeonekana kuwa mkuu kuliko wote miongoni mwao. 25Yesu akawaambia, “Wafalme na watu wa Mataifa huwatawala watu kwa nguvu. Nao wenye mamlaka juu yao hujiita ‘Wafadhili.’ 26Lakini ninyi msifanane nao. Bali yeye aliye mkuu kuliko wote miongoni mwenu, inampasa kuwa kama yeye aliye mdogo wa wote, naye atawalaye na awe kama yeye ahudumuye. 27Kwani ni nani aliye mkuu? Ni yule aketiye mezani au ni yule ahudumuye? Si ni yule aliyekaa mezani? Lakini mimi niko miongoni mwenu kama yule ahudumuye. 28Ninyi mmekuwa pamoja nami katika majaribu yangu. 29Nami kama Baba yangu alivyonipa ufalme, kadhalika mimi nami ninawapa ninyi, 30ili mpate kula na kunywa mezani pangu katika karamu ya ufalme wangu, na kukaa katika viti vya enzi, mkihukumu makabila kumi na mawili ya Israeli.” 31Yesu akasema, “Simoni, Simoni, sikiliza, Shetani ameomba kuwapepeta ninyi wote kama ngano. 32Lakini nimekuombea wewe Simoni ili imani yako isishindwe, nawe ukiisha kunirudia, uwaimarishe ndugu zako.” 33Petro akajibu, “Bwana, niko tayari kwenda pamoja nawe gerezani na hata kifoni.” 34Yesu akamjibu, “Ninakuambia Petro, kabla jogoo hajawika usiku wa leo, utakana mara tatu kwamba hunijui mimi.” 35Kisha Yesu akawauliza, “Nilipowatuma bila mfuko, wala mkoba, wala viatu, mlipungukiwa na kitu chochote?” Wakajibu, “La, hatukupungukiwa na kitu chochote.” 36Akawaambia, “Lakini sasa, aliye na mfuko na auchukue, na aliye na mkoba vivyo hivyo. Naye asiye na upanga, auze joho lake anunue mmoja. 37Kwa sababu, nawaambia, andiko hili lazima litimizwe juu yangu, kwamba, ‘Alihesabiwa pamoja na wakosaji’; kwa kweli yaliyoandikwa kunihusu mimi hayana budi kutimizwa.” 38Wanafunzi wake wakamwambia, “Bwana, tazama hapa kuna panga mbili.” Akawajibu, “Inatosha.” 39Yesu akatoka, akaenda kwenye Mlima wa Mizeituni kama ilivyokuwa kawaida yake, nao wanafunzi wake wakamfuata. 40Walipofika huko, akawaambia wanafunzi wake, “Ombeni, msije mkaingia majaribuni.” 41Akajitenga nao kama umbali wa kutupa jiwe, akapiga magoti, akaomba 42akisema, “Baba, kama ni mapenzi yako, niondolee kikombe hiki. Lakini si kama nipendavyo, bali mapenzi yako yatendeke.” 43Malaika kutoka mbinguni akamtokea, akamtia nguvu. 44Naye akiwa katika maumivu makuu, akaomba kwa bidii, nalo jasho lake likawa kama matone ya damu yakidondoka ardhini. 45Baada ya kuomba, akawarudia wanafunzi wake akawakuta wamelala, wakiwa wamechoka kutokana na huzuni. 46Naye akawauliza, “Mbona mmelala? Amkeni, mwombe ili msije mkaingia majaribuni.” 47Yesu alipokuwa bado anazungumza, umati mkubwa wa watu ukaja. Uliongozwa na Yuda, ambaye alikuwa mmoja wa wale wanafunzi Kumi na Wawili. Akamkaribia Yesu ili ambusu. 48Lakini Yesu akamwambia, “Yuda, je, unamsaliti Mwana wa Adamu kwa busu?” 49Wafuasi wa Yesu walipoona yale yaliyokuwa yanakaribia kutokea, wakasema, “Bwana, tuwakatekate kwa panga zetu?” 50Mmoja wao akampiga mtumishi wa kuhani mkuu kwa upanga, akamkata sikio la kuume. 51Lakini Yesu akasema, “Acheni!” Akaligusa lile sikio la yule mtu na kumponya. 52Kisha Yesu akawaambia wale viongozi wa makuhani, maafisa wa walinzi wa Hekalu, pamoja na wazee waliokuwa wamekuja kumkamata, “Mmekuja na panga na marungu, kana kwamba mimi ni mnyangʼanyi? 53Siku kwa siku nilikuwa pamoja nanyi Hekaluni lakini hamkunikamata. Lakini hii ni saa yenu, wakati giza linatawala!” 54Kisha wakamkamata Yesu, wakamchukua, wakaenda naye mpaka nyumbani kwa kuhani mkuu. Lakini Petro akafuata kwa mbali. 55Walipokwisha kuwasha moto katikati ya ua na kuketi pamoja, Petro naye akaketi pamoja nao. 56Mtumishi mmoja wa kike akamwona kwa mwanga wa moto akiwa ameketi pale. Akamtazama sana, akasema, “Huyu mtu pia alikuwa pamoja na Yesu!” 57Lakini Petro akakana, akasema, “Ewe mwanamke, hata simjui!” 58Baadaye kidogo, mtu mwingine alimwona Petro akasema, “Wewe pia ni mmoja wao!” Petro akajibu, “Wewe mtu, mimi sio mmoja wao!” 59Baada ya muda wa kama saa moja hivi, mtu mwingine akazidi kusisitiza, “Kwa hakika huyu mtu naye alikuwa pamoja na Yesu, kwa maana yeye pia ni Mgalilaya.” 60Petro akajibu, “Wewe mtu, mimi sijui unalosema!” Wakati huo huo, akiwa bado anazungumza, jogoo akawika. 61Naye Bwana akageuka, akamtazama Petro. Ndipo Petro akakumbuka lile neno ambalo Bwana alimwambia: “Kabla jogoo hajawika leo, utanikana mara tatu.” 62Naye akaenda nje, akalia kwa majonzi. 63Watu waliokuwa wanamlinda Yesu wakaanza kumdhihaki na kumpiga. 64Wakamfunga kitambaa machoni na kumuuliza, “Tabiri! Tuambie ni nani aliyekupiga?” 65Wakaendelea kumtukana kwa matusi mengi. 66Kulipopambazuka, baraza la wazee wa watu, yaani viongozi wa makuhani na walimu wa sheria, wakakutana pamoja, naye Yesu akaletwa mbele yao. 67Wakamwambia, “Kama wewe ndiye Kristo, tuambie.” Yesu akawajibu, “Hata nikiwaambia hamtaamini. 68Nami nikiwauliza swali, hamtanijibu. 69Lakini kuanzia sasa, Mwana wa Adamu ataketi mkono wa kuume wa Mungu Mwenye Nguvu.” 70Wote wakauliza, “Wewe basi ndiwe Mwana wa Mungu?” Yeye akawajibu, “Ninyi mwasema kwamba mimi ndiye.” 71Kisha wakasema, “Tuna haja gani tena ya ushahidi zaidi? Tumesikia wenyewe kutoka kinywani mwake.”
1Now the feast of unleavened bread, which is called the Passover, drew near. 2The chief priests and the scribes sought how they might put him to death, for they feared the people. 3Satan entered into Judas, who was also called Iscariot, who was numbered with the twelve. 4He went away, and talked with the chief priests and captains about how he might deliver him to them. 5They were glad, and agreed to give him money. 6He consented, and sought an opportunity to deliver him to them in the absence of the multitude. 7The day of unleavened bread came, on which the Passover must be sacrificed. 8He sent Peter and John, saying, “Go and prepare the Passover for us, that we may eat.” 9They said to him, “Where do you want us to prepare?” 10He said to them, “Behold, when you have entered into the city, a man carrying a pitcher of water will meet you. Follow him into the house which he enters. 11Tell the master of the house, ‘The Teacher says to you, “Where is the guest room, where I may eat the Passover with my disciples?”’ 12He will show you a large, furnished upper room. Make preparations there.” 13They went, found things as he had told them, and they prepared the Passover. 14When the hour had come, he sat down with the twelve apostles. 15He said to them, “I have earnestly desired to eat this Passover with you before I suffer, 16for I tell you, I will no longer by any means eat of it until it is fulfilled in the Kingdom of God.” 17He received a cup, and when he had given thanks, he said, “Take this, and share it among yourselves, 18for I tell you, I will not drink at all again from the fruit of the vine, until the Kingdom of God comes.” 19He took bread, and when he had given thanks, he broke it, and gave to them, saying, “This is my body which is given for you. Do this in memory of me.” 20Likewise, he took the cup after supper, saying, “This cup is the new covenant in my blood, which is poured out for you. 21But behold, the hand of him who betrays me is with me on the table. 22The Son of Man indeed goes, as it has been determined, but woe to that man through whom he is betrayed!” 23They began to question among themselves, which of them it was who would do this thing. 24There arose also a contention among them, which of them was considered to be greatest. 25He said to them, “The kings of the nations lord it over them, and those who have authority over them are called ‘benefactors.’ 26But not so with you. But one who is the greater among you, let him become as the younger, and one who is governing, as one who serves. 27For who is greater, one who sits at the table, or one who serves? Isn’t it he who sits at the table? But I am in your midst as one who serves. 28But you are those who have continued with me in my trials. 29I confer on you a kingdom, even as my Father conferred on me, 30that you may eat and drink at my table in my Kingdom. You will sit on thrones, judging the twelve tribes of Israel.” 31The Lord said, “Simon, Simon, behold, Satan asked to have you, that he might sift you as wheat, 32but I prayed for you, that your faith wouldn’t fail. You, when once you have turned again, establish your brothers.” 33He said to him, “Lord, I am ready to go with you both to prison and to death!” 34He said, “I tell you, Peter, the rooster will by no means crow today until you deny that you know me three times.” 35He said to them, “When I sent you out without purse, and wallet, and shoes, did you lack anything?” They said, “Nothing.” 36Then he said to them, “But now, whoever has a purse, let him take it, and likewise a wallet. Whoever has none, let him sell his cloak, and buy a sword. 37For I tell you that this which is written must still be fulfilled in me: ‘He was counted with transgressors.’ For that which concerns me has an end.” 38They said, “Lord, behold, here are two swords.” He said to them, “That is enough.” 39He came out, and went, as his custom was, to the Mount of Olives. His disciples also followed him. 40When he was at the place, he said to them, “Pray that you don’t enter into temptation.” 41He was withdrawn from them about a stone’s throw, and he knelt down and prayed, 42saying, “Father, if you are willing, remove this cup from me. Nevertheless, not my will, but yours, be done.” 43An angel from heaven appeared to him, strengthening him. 44Being in agony he prayed more earnestly. His sweat became like great drops of blood falling down on the ground. 45When he rose up from his prayer, he came to the disciples, and found them sleeping because of grief, 46and said to them, “Why do you sleep? Rise and pray that you may not enter into temptation.” 47While he was still speaking, behold, a multitude, and he who was called Judas, one of the twelve, was leading them. He came near to Jesus to kiss him. 48But Jesus said to him, “Judas, do you betray the Son of Man with a kiss?” 49When those who were around him saw what was about to happen, they said to him, “Lord, shall we strike with the sword?” 50A certain one of them struck the servant of the high priest, and cut off his right ear. 51But Jesus answered, “Let me at least do this”—and he touched his ear, and healed him. 52Jesus said to the chief priests, captains of the temple, and elders, who had come against him, “Have you come out as against a robber, with swords and clubs? 53When I was with you in the temple daily, you didn’t stretch out your hands against me. But this is your hour, and the power of darkness.” 54They seized him, and led him away, and brought him into the high priest’s house. But Peter followed from a distance. 55When they had kindled a fire in the middle of the courtyard, and had sat down together, Peter sat among them. 56A certain servant girl saw him as he sat in the light, and looking intently at him, said, “This man also was with him.” 57He denied Jesus, saying, “Woman, I don’t know him.” 58After a little while someone else saw him, and said, “You also are one of them!” But Peter answered, “Man, I am not!” 59After about one hour passed, another confidently affirmed, saying, “Truly this man also was with him, for he is a Galilean!” 60But Peter said, “Man, I don’t know what you are talking about!” Immediately, while he was still speaking, a rooster crowed. 61The Lord turned, and looked at Peter. Then Peter remembered the Lord’s word, how he said to him, “Before the rooster crows you will deny me three times.” 62He went out, and wept bitterly. 63The men who held Jesus mocked him and beat him. 64Having blindfolded him, they struck him on the face and asked him, “Prophesy! Who is the one who struck you?” 65They spoke many other things against him, insulting him. 66As soon as it was day, the assembly of the elders of the people was gathered together, both chief priests and scribes, and they led him away into their council, saying, 67“If you are the Christ, tell us.” But he said to them, “If I tell you, you won’t believe, 68and if I ask, you will in no way answer me or let me go. 69From now on, the Son of Man will be seated at the right hand of the power of God.” 70They all said, “Are you then the Son of God?” He said to them, “You say it, because I am.” 71They said, “Why do we need any more witness? For we ourselves have heard from his own mouth!”
1En het feest der ongehevelde broden, genaamd pascha, was nabij. 2En de overpriesters en de Schriftgeleerden zochten, hoe zij Hem ombrengen zouden; want zij vreesden het volk. 3En de satan voer in Judas, die toegenaamd was Iskariot, zijnde uit het getal der twaalven. 4En hij ging heen en sprak met de overpriesters en de hoofdmannen, hoe hij Hem hun zou overleveren. 5En zij waren verblijd, en zijn het eens geworden, dat zij hem geld geven zouden. 6En hij beloofde het, en zocht gelegenheid, om Hem hun over te leveren, zonder oproer. 7En de dag der ongehevelde broden kwam, op denwelken het pascha moest geslacht worden. 8En Hij zond Petrus en Johannes uit, zeggende: Gaat heen, en bereidt ons het pascha, opdat wij het eten mogen. 9En zij zeiden tot Hem: Waar wilt Gij, dat wij het bereiden? 10En Hij zeide tot hen: Ziet, als gij in de stad zult gekomen zijn, zo zal u een mens ontmoeten, dragende een kruik waters; volgt hem in het huis, daar hij ingaat. 11En gij zult zeggen tot den huisvader van dat huis: De Meester zegt u: Waar is de eetzaal, daar Ik het pascha met Mijn discipelen eten zal? 12En hij zal u een grote toegeruste opperzaal wijzen, bereidt het aldaar. 13En zij, heengaande, vonden het, gelijk Hij hun gezegd had, en bereidden het pascha. 14En als de ure gekomen was, zat Hij aan, en de twaalf apostelen met Hem. 15En Hij zeide tot hen: Ik heb grotelijks begeerd, dit pascha met u te eten, eer dat Ik lijde; 16Want Ik zeg u, dat Ik niet meer daarvan eten zal, totdat het vervuld zal zijn in het Koninkrijk Gods. 17En als Hij een drinkbeker genomen had, en gedankt had, zeide Hij: Neemt dezen, en deelt hem onder ulieden. 18Want Ik zeg u, dat Ik niet drinken zal van de vrucht des wijnstoks, totdat het Koninkrijk Gods zal gekomen zijn. 19En Hij nam brood, en als Hij gedankt had, brak Hij het, en gaf het hun, zeggende: Dat is Mijn lichaam, hetwelk voor u gegeven wordt; doet dat tot Mijn gedachtenis. 20Desgelijks ook den drinkbeker na het avondmaal, zeggende: Deze drinkbeker is het nieuwe testament in Mijn bloed, hetwelk voor u vergoten wordt. 21Doch ziet, de hand desgenen, die Mij verraadt, is met Mij aan de tafel. 22En de Zoon des mensen gaat wel heen, gelijk besloten is; doch wee dien mens, door welken Hij verraden wordt! 23En zij begonnen onder elkander te vragen, wie van hen het toch mocht zijn, die dat doen zou. 24En er werd ook twisting onder hen, wie van hen scheen de meeste te zijn. 25En Hij zeide tot hen: De koningen der volken heersen over hen; en die macht over hen hebben, worden weldadige heren genaamd. 26Doch gij niet alzo; maar de meeste onder u, die zij gelijk de minste, en die voorganger is, als een die dient. 27Want wie is meerder, die aanzit, of die dient? Is het niet die aanzit? Maar Ik ben in het midden van u, als een die dient. 28En gij zijt degenen, die met Mij steeds gebleven zijt in Mijn verzoekingen. 29En Ik verordineer u het Koninkrijk, gelijkerwijs Mijn Vader dat Mij verordineerd heeft; 30Opdat gij eet en drinkt aan Mijn tafel in Mijn Koninkrijk, en zit op tronen, oordelende de twaalf geslachten Israels. 31En de Heere zeide: Simon, Simon, ziet, de satan heeft ulieden zeer begeerd om te ziften als de tarwe; 32Maar Ik heb voor u gebeden, dat uw geloof niet ophoude; en gij, als gij eens zult bekeerd zijn, zo versterk uw broeders. 33En hij zeide tot Hem: Heere, ik ben bereid, met U ook in de gevangenis en in den dood te gaan. 34Maar Hij zeide: Ik zeg u, Petrus, de haan zal heden niet kraaien, eer gij driemaal zult verloochend hebben, dat gij Mij kent. 35En Hij zeide tot hen: Als Ik u uitzond, zonder buidel, en male, en schoenen, heeft u ook iets ontbroken? En zij zeiden: Niets. 36Hij zeide dan tot hen: Maar nu, wie een buidel heeft, die neme hem, desgelijks ook een male; en die geen heeft, die verkope zijn kleed, en kope een zwaard. 37Want Ik zeg u, dat nog dit, hetwelk geschreven is, in Mij moet volbracht worden, namelijk: En Hij is met de misdadigen gerekend. Want ook die dingen, die van Mij geschreven zijn, hebben een einde. 38En zij zeiden: Heere! zie hier twee zwaarden. En Hij zeide tot hen: Het is genoeg. 39En uitgaande, vertrok Hij, gelijk Hij gewoon was, naar den Olijfberg; en Hem volgden ook Zijn discipelen. 40En als Hij aan die plaats gekomen was, zeide Hij tot hen: Bidt, dat gij niet in verzoeking komt. 41En Hij scheidde Zich van hen af, omtrent een steenworp; en knielde neder en bad, 42Zeggende: Vader, of Gij wildet dezen drinkbeker van Mij wegnemen, doch niet Mijn wil, maar de Uwe geschiede. 43En van Hem werd gezien een engel uit den hemel, die Hem versterkte. 44En in zwaren strijd zijnde, bad Hij te ernstiger. En zijn zweet werd gelijk grote droppelen bloeds, die op de aarde afliepen. 45En als Hij van het gebed opgestaan was, kwam Hij tot Zijn discipelen, en vond hen slapende van droefheid. 46En Hij zeide tot hen: Wat slaapt gij? Staat op en bidt, opdat gij niet in verzoeking komt. 47En als Hij nog sprak, ziet daar een schare; en een van de twaalven, die genaamd was Judas, ging hun voor, en kwam bij Jezus, om Hem te kussen. 48En Jezus zeide tot hem: Judas, verraadt gij den Zoon des mensen met een kus? 49En die bij Hem waren, ziende, wat er geschieden zou, zeiden tot Hem: Heere, zullen wij met het zwaard slaan? 50En een uit hen sloeg den dienstknecht des hogepriesters, en hieuw hem zijn rechteroor af. 51En Jezus, antwoordende, zeide: Laat hen tot hiertoe geworden; en raakte zijn oor aan, en heelde hem. 52En Jezus zeide tot de overpriesters, en de hoofdmannen des tempels, en ouderlingen, die tegen Hem gekomen waren: Zijt gij uitgegaan met zwaarden en stokken als tegen een moordenaar? 53Als Ik dagelijks met u was in den tempel, zo hebt gij de handen tegen Mij niet uitgestoken; maar dit is uw ure, en de macht der duisternis. 54En zij grepen Hem en leidden Hem weg, en brachten Hem in het huis des hogepriesters. En Petrus volgde van verre. 55En als zij vuur ontstoken hadden in het midden van de zaal, en zij te zamen nederzaten, zat Petrus in het midden van hen. 56En een zekere dienstmaagd, ziende hem bij het vuur zitten, en haar ogen op hem houdende, zeide: Ook deze was met Hem. 57Maar hij verloochende Hem, zeggende: Vrouw, ik ken Hem niet. 58En kort daarna een ander, hem ziende, zeide: Ook gij zijt van die. Maar Petrus zeide: Mens, ik ben niet. 59En als het omtrent een uur geleden was, bevestigde dat een ander, zeggende: In der waarheid, ook deze was met Hem; want hij is ook een Galileer. 60Maar Petrus zeide: Mens, ik weet niet, wat gij zegt. En terstond, als hij nog sprak, kraaide de haan. 61En de Heere, Zich omkerende, zag Petrus aan; en Petrus werd indachtig het woord des Heeren, hoe Hij hem gezegd had: Eer de haan zal gekraaid hebben, zult gij Mij driemaal verloochenen. 62En Petrus, naar buiten gaande, weende bitterlijk. 63En de mannen, die Jezus hielden, bespotten Hem, en sloegen Hem. 64En als zij Hem overdekt hadden, sloegen zij Hem op het aangezicht, en vraagden Hem, zeggende: Profeteer, wie het is, die U geslagen heeft? 65En vele andere dingen zeiden zij tegen Hem, lasterende. 66En als het dag geworden was, vergaderden de ouderlingen des volks, en de overpriesters en Schriftgeleerden, en brachten Hem in hun raad, 67Zeggende: Zijt Gij de Christus, zeg het ons. En Hij zeide tot hen: Indien Ik het u zeg, gij zult het niet geloven; 68En indien Ik ook vraag, gij zult Mij niet antwoorden, of loslaten; 69Van nu aan zal de Zoon des mensen gezeten zijn aan de rechter hand der kracht Gods. 70En zij zeiden allen: Zijt Gij dan de Zoon Gods? En Hij zeide tot hen: Gij zegt, dat Ik het ben. 71En zij zeiden: Wat hebben wij nog getuigenis van node? Want wij zelven hebben het uit Zijn mond gehoord.
Bonyeza Enter ili kuuwekea mstari huu rangi, kuandika maelezo au kuunakili. Vitufe vya mishale vinakupeleka kwenye mstari unaofuata.
Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.