1Basi viongozi wa jamaa ya Walawi, wakamwendea kuhani Eleazari, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa jamaa nyingine za makabila ya Israeli 2huko Shilo katika Kanaani na kuwaambia, “Bwana aliamuru kupitia Mose kuwa mtupe miji ya kuishi yenye sehemu za malisho kwa mifugo yetu.” 3Hivyo kama vile Bwana alivyoamuru, Waisraeli wakawapa Walawi miji ifuatayo pamoja na sehemu zake za malisho kutoka urithi wao wenyewe. 4Kura ya kwanza ikaangukia Wakohathi, ukoo kwa ukoo. Walawi waliokuwa wazao wa kuhani Aroni walipewa miji kumi na mitatu kutoka makabila ya Yuda, Simeoni na Benyamini. 5Wazao wengine waliobaki wa Wakohathi walipewa miji kumi kutoka koo za makabila ya Efraimu, Dani na nusu ya Manase. 6Wazao wa Gershoni walipewa miji kumi na mitatu kutoka koo za makabila ya Isakari, Asheri, Naftali na nusu ya Manase huko Bashani. 7Wazao wa Merari, ukoo kwa ukoo, walipewa miji kumi na miwili kutoka makabila ya Reubeni, Gadi na Zabuloni. 8Kwa hiyo Waisraeli wakawapa Walawi miji hii pamoja na sehemu zake za malisho, kama vile Bwana alivyokuwa ameamuru kupitia kwa Mose. 9Kutoka makabila ya Yuda na Simeoni waligawa miji ifuatayo kwa majina 10(miji hii walipewa wazao wa Aroni ambao walitokana na koo za Wakohathi wa Walawi, kwa sababu kura ya kwanza iliwaangukia): 11Waliwapa Kiriath-Arba (yaani Hebroni), pamoja na sehemu zake za malisho zilizoizunguka, katika nchi ya vilima ya Yuda. (Arba alikuwa baba wa Anaki.) 12Lakini mashamba na vijiji vilivyozunguka mji mkubwa walikuwa wamempa Kalebu mwana wa Yefune kuwa milki yake. 13Kwa hiyo wazao wa kuhani Aroni wakapewa Hebroni (mji mkuu wa makimbilio kwa ajili ya yeyote aliyeshtakiwa kwa mauaji), Libna, 14Yatiri, Eshtemoa, 15Holoni, Debiri, 16Aini, Yuta na Beth-Shemeshi, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji tisa kutoka kwa makabila haya mawili. 17Kutoka kabila la Benyamini wakawapa Gibeoni, Geba, 18Anathothi na Almoni, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne. 19Miji yote waliyopewa makuhani, wazao wa Aroni, ilikuwa kumi na mitatu, pamoja na sehemu zake za malisho. 20Koo nyingine za Wakohathi, ambao pia ni Walawi, walipewa miji kutoka kabila la Efraimu: 21Katika nchi ya vilima ya Efraimu walipewa Shekemu (mji mkubwa wa makimbilio kwa yeyote anayeshtakiwa kwa mauaji) na Gezeri, 22Kibsaimu na Beth-Horoni, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne. 23Pia kutoka kabila la Dani wakapokea Elteke, Gibethoni, 24Aiyaloni na Gath-Rimoni pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne 25Kutoka nusu ya kabila la Manase, wakapokea Taanaki na Gath-Rimoni pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji miwili. 26Miji yote hii kumi pamoja na sehemu zake za malisho ilipewa koo za Wakohathi zilizobaki. 27Koo za Walawi za Wagershoni walipewa: kutoka nusu ya kabila la Manase, Golani katika Bashani (mji mkuu wa makimbilio kwa yeyote aliyeshtakiwa kwa mauaji) na Beeshtera, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji miwili; 28kutoka kabila la Isakari walipewa, Kishioni, Daberathi, 29Yarmuthi na En-Ganimu, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne 30kutoka kabila la Asheri walipewa, Mishali, Abdoni, 31Helkathi na Rehobu, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne. 32Kutoka kabila la Naftali walipewa, Kedeshi katika Galilaya (mji wa makimbilio kwa ajili ya yeyote anayeshtakiwa kwa mauaji), Hamoth-Dori na Kartani, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji mitano. 33Miji yote ya koo za Wagershoni ilikuwa kumi na mitatu, pamoja na sehemu zake za malisho. 34Koo za Wamerari (Walawi waliobaki) walipewa: kutoka kabila la Zabuloni, Yokneamu, Karta, 35Dimna na Nahalali, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne; 36kutoka kabila la Reubeni walipewa Bezeri, Yahasa, 37Kedemothi na Mefaathi, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne; 38kutoka kabila la Gadi walipewa, Ramothi katika Gileadi (mji wa makimbilio kwa ajili ya yeyote anayeshtakiwa kwa ajili ya mauaji), Mahanaimu, 39Heshboni na Yazeri, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne. 40Miji yote waliyopewa koo za Wamerari, waliokuwa mabaki ya Walawi, ilikuwa ni kumi na miwili. 41Miji yote ya Walawi katika eneo lililoshikwa na Waisraeli lilikuwa arobaini na minane, pamoja na sehemu zake za malisho. 42Kila mmoja wa miji hii ulikuwa na sehemu ya malisho kuuzunguka; ndivyo ilivyokuwa kwa miji hii yote. 43Kwa hiyo Bwana akawapa Israeli nchi yote aliyokuwa ameapa kuwapa baba zao, nao wakaimiliki na kukaa humo. 44Bwana akawapa pumziko kila upande, kama vile alivyokuwa amewaapia baba zao, hakuna hata mmoja wa adui zao aliyeweza kusimama mbele yao, Bwana akawatia adui zao wote mikononi mwao. 45Hakuna hata mojawapo ya ahadi nzuri ya Bwana kwa nyumba ya Israeli ambayo haikutimia; kila moja ilitimia.
1Then the heads of fathers’ houses of the Levites came near to Eleazar the priest, and to Joshua the son of Nun, and to the heads of fathers’ houses of the tribes of the children of Israel. 2They spoke to them at Shiloh in the land of Canaan, saying, “Yahweh commanded Moses to give us cities to dwell in, with their suburbs for our livestock.” 3The children of Israel gave to the Levites out of their inheritance, according to the commandment of Yahweh, these cities with their suburbs. 4The lot came out for the families of the Kohathites. The children of Aaron the priest, who were of the Levites, had thirteen cities by lot out of the tribe of Judah, out of the tribe of the Simeonites, and out of the tribe of Benjamin. 5The rest of the children of Kohath had ten cities by lot out of the families of the tribe of Ephraim, out of the tribe of Dan, and out of the half-tribe of Manasseh. 6The children of Gershon had thirteen cities by lot out of the families of the tribe of Issachar, out of the tribe of Asher, out of the tribe of Naphtali, and out of the half-tribe of Manasseh in Bashan. 7The children of Merari according to their families had twelve cities out of the tribe of Reuben, out of the tribe of Gad, and out of the tribe of Zebulun. 8The children of Israel gave these cities with their suburbs by lot to the Levites, as Yahweh commanded by Moses. 9They gave out of the tribe of the children of Judah, and out of the tribe of the children of Simeon, these cities which are mentioned by name: 10and they were for the children of Aaron, of the families of the Kohathites, who were of the children of Levi; for theirs was the first lot. 11They gave them Kiriath Arba, named after the father of Anak (the same is Hebron), in the hill country of Judah, with its suburbs around it. 12But they gave the fields of the city and its villages to Caleb the son of Jephunneh for his possession. 13To the children of Aaron the priest they gave Hebron with its suburbs, the city of refuge for the man slayer, Libnah with its suburbs, 14Jattir with its suburbs, Eshtemoa with its suburbs, 15Holon with its suburbs, Debir with its suburbs, 16Ain with its suburbs, Juttah with its suburbs, and Beth Shemesh with its suburbs; nine cities out of those two tribes. 17Out of the tribe of Benjamin, Gibeon with its suburbs, Geba with its suburbs, 18Anathoth with its suburbs, and Almon with its suburbs; four cities. 19All the cities of the children of Aaron, the priests, were thirteen cities with their suburbs. 20The families of the children of Kohath, the Levites, even the rest of the children of Kohath, had the cities of their lot out of the tribe of Ephraim. 21They gave them Shechem with its suburbs in the hill country of Ephraim, the city of refuge for the man slayer, and Gezer with its suburbs, 22Kibzaim with its suburbs, and Beth Horon with its suburbs; four cities. 23Out of the tribe of Dan, Elteke with its suburbs, Gibbethon with its suburbs, 24Aijalon with its suburbs, Gath Rimmon with its suburbs; four cities. 25Out of the half-tribe of Manasseh, Taanach with its suburbs, and Gath Rimmon with its suburbs; two cities. 26All the cities of the families of the rest of the children of Kohath were ten with their suburbs. 27They gave to the children of Gershon, of the families of the Levites, out of the half-tribe of Manasseh Golan in Bashan with its suburbs, the city of refuge for the man slayer, and Be Eshterah with its suburbs; two cities. 28Out of the tribe of Issachar, Kishion with its suburbs, Daberath with its suburbs, 29Jarmuth with its suburbs, En Gannim with its suburbs; four cities. 30Out of the tribe of Asher, Mishal with its suburbs, Abdon with its suburbs, 31Helkath with its suburbs, and Rehob with its suburbs; four cities. 32Out of the tribe of Naphtali, Kedesh in Galilee with its suburbs, the city of refuge for the man slayer, Hammothdor with its suburbs, and Kartan with its suburbs; three cities. 33All the cities of the Gershonites according to their families were thirteen cities with their suburbs. 34To the families of the children of Merari, the rest of the Levites, out of the tribe of Zebulun, Jokneam with its suburbs, Kartah with its suburbs, 35Dimnah with its suburbs, and Nahalal with its suburbs; four cities. 36Out of the tribe of Reuben, Bezer with its suburbs, Jahaz with its suburbs, 37Kedemoth with its suburbs, and Mephaath with its suburbs; four cities. 38Out of the tribe of Gad, Ramoth in Gilead with its suburbs, the city of refuge for the man slayer, and Mahanaim with its suburbs, 39Heshbon with its suburbs, Jazer with its suburbs; four cities in all. 40All these were the cities of the children of Merari according to their families, even the rest of the families of the Levites. Their lot was twelve cities. 41All the cities of the Levites in the midst of the possession of the children of Israel were forty-eight cities with their suburbs. 42Each of these cities included their suburbs around them. It was this way with all these cities. 43So Yahweh gave to Israel all the land which he swore to give to their fathers. They possessed it, and lived in it. 44Yahweh gave them rest all around, according to all that he swore to their fathers. Not a man of all their enemies stood before them. Yahweh delivered all their enemies into their hand. 45Nothing failed of any good thing which Yahweh had spoken to the house of Israel. All came to pass.
1Toen naderden de hoofden der vaderen van de Levieten tot Eleazar, den priester, en tot Jozua, den zoon van Nun, en tot de hoofden der vaderen van de stammen der kinderen Israels; 2En zij spraken tot hen, te Silo, in het land Kanaan, zeggende: De HEERE heeft geboden door den dienst van Mozes, dat men ons steden te bewonen geven zou, en haar voorsteden voor onze beesten. 3Daarom gaven de kinderen Israels aan de Levieten van hun erfdeel, naar den mond des HEEREN, deze steden en de voorsteden derzelve. 4Toen ging het lot uit voor de huisgezinnen der Kahathieten; en voor de kinderen van Aaron, den priester, uit de Levieten, waren van den stam van Juda, en van den stam van Simeon, en van den stam van Benjamin, door het lot, dertien steden. 5En aan de overgebleven kinderen van Kahath vielen, bij het lot, van de huisgezinnen van den stam van Efraim, en van den stam van Dan, en van den halven stam van Manasse, tien steden. 6En aan den kinderen van Gerson, van de huisgezinnen van den stam van Issaschar, en van den stam van Aser, en van den stam van Nafthali, en van den halven stam van Manasse, in Bazan, bij het lot, dertien steden. 7Aan de kinderen van Merari, naar hun huisgezinnen, van den stam van Ruben, en van den stam van Gad, en van den stam van Zebulon, twaalf steden. 8Alzo gaven de kinderen Israels aan de Levieten deze steden en haar voorsteden, bij het lot, gelijk de HEERE geboden had door den dienst van Mozes. 9Verder gaven zij van den stam der kinderen van Juda, en van den stam der kinderen van Simeon, deze steden, die men bij name noemde; 10Dat zij waren van de kinderen van Aaron, van de huisgezinnen der Kahathieten, uit de kinderen van Levi; want het eerste lot was het hunne. 11Zo gaven zij hun de stad van Arba, den vader van Anok (zij is Hebron), op den berg van Juda, en haar voorsteden rondom haar. 12Maar het veld der stad en haar dorpen, gaven zij aan Kaleb, den zoon van Jefunne, tot zijn bezitting. 13Alzo gaven zij aan de kinderen van den priester Aaron de vrijstad des doodslagers, Hebron en haar voorsteden, en Libna en haar voorsteden; 14En Jatthir en haar voorsteden, en Esthemoa en haar voorsteden; 15En Holon en haar voorsteden, en Debir en haar voorsteden; 16En Ain en haar voorsteden, en Jutta en haar voorsteden, en Beth-Semes en haar voorsteden; negen steden van deze twee stammen. 17En van den stam van Benjamin, Gibeon en haar voorsteden, Geba en haar voorsteden; 18Anathoth en haar voorsteden, en Almon en haar voorsteden: vier steden. 19Al de steden der kinderen van Aaron, de priesteren, waren dertien steden en haar voorsteden. 20De huisgezinnen nu der kinderen van Kahath, de Levieten, die overgebleven waren van de kinderen van Kahath, die hadden de steden huns lots van den stam van Efraim. 21En zij gaven hun Sichem, een vrijstad des doodslagers, en haar voorsteden, op den berg Efraim, en Gezer en haar voorsteden; 22En Kibzaim en haar voorsteden, en Beth-horon en haar voorsteden: vier steden. 23En van den stam van Dan, Elteke en haar voorsteden, Gibbethon en haar voorsteden; 24Ajalon en haar voorsteden, Gath-Rimmon en haar voorsteden: vier steden. 25En van den halven stam van Manasse, Thaanach en haar voorsteden, en Gath-Rimmon en haar voorsteden: twee steden. 26Al de steden voor de huisgezinnen van de overige kinderen van Kahath zijn tien, met haar voorsteden. 27En aan de kinderen van Gerson, van de huisgezinnen der Levieten, van den halven stam van Manasse, de vrijstad des doodslagers, Golan in Bazan, en haar voorsteden, en Beesthera en haar voorsteden: twee steden. 28En van den stam van Issaschar, Kisjon en haar voorsteden, en Dobrath en haar voorsteden; 29Jarmuth en haar voorsteden, En-gannim en haar voorsteden: vier steden. 30En van den stam van Aser, Misal en haar voorsteden, Abdon en haar voorsteden; 31En Helkath en haar voorsteden, en Rehob en haar voorsteden: vier steden. 32En van den stam van Nafthali, de vrijstad des doodslagers, Kedes in Galilea, en haar voorsteden, en Hammoth-Dor en haar voorsteden, en Karthan en haar voorsteden: drie steden. 33Al de steden der Gersonieten, naar hun huisgezinnen, zijn dertien steden en haar voorsteden. 34Aan de huisgezinnen nu van de kinderen van Merari, van de overige Levieten, werd gegeven van den stam van Zebulon, Jokneam en haar voorsteden, Kartha en haar voorsteden; 35Dimna en haar voorsteden, Nahalal en haar voorsteden: vier steden. 36En van den stam van Ruben, Bezer en haar voorsteden, en Jahza en haar voorsteden; 37Kedemoth en haar voorsteden, en Mefaath en haar voorsteden: vier steden. 38Van den stam van Gad nu, de vrijstad des doodslagers, Ramoth in Gilead, en haar voorsteden, en Mahanaim en haar voorsteden; 39Hesbon en haar voorsteden, Jaezer en haar voorsteden: al die steden zijn vier. 40Al die steden waren van de kinderen van Merari, naar hun huisgezinnen, die nog overig waren van de huisgezinnen der Levieten; en hun lot was twaalf steden. 41Al de steden der Levieten, in het midden van de erfenis der kinderen Israels, waren acht en veertig steden en haar voorsteden. 42Deze steden waren elk met haar voorsteden rondom haar; alzo was het met al die steden. 43Alzo gaf de HEERE aan Israel het ganse land, dat Hij gezworen had hun vaderen te geven, en zij beerfden het, en woonden daarin. 44En de HEERE gaf hun rust rondom, naar alles, wat Hij hun vaderen gezworen had; en er bestond niet een man van al hun vijanden voor hun aangezicht; al hun vijanden gaf de HEERE in hun hand. 45Er viel niet een woord van al de goede woorden, die de HEERE gesproken had tot het huis van Israel; het kwam altemaal.
Bonyeza Enter ili kuuwekea mstari huu rangi, kuandika maelezo au kuunakili. Vitufe vya mishale vinakupeleka kwenye mstari unaofuata.
Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.