1Makabila yote ya Israeli yakamjia Daudi huko Hebroni na kumwambia, “Sisi tu nyama yako na damu yako hasa. 2Zamani, wakati Sauli alikuwa mfalme juu yetu, wewe ndiwe uliyeiongoza Israeli vitani. Naye Bwana alikuambia, ‘Wewe utawachunga watu wangu Israeli, na utakuwa mtawala wao.’” 3Wazee wote wa Israeli wakamwendea Mfalme Daudi huko Hebroni, mfalme akafanya mapatano nao huko Hebroni mbele za Bwana, nao wakamtia Daudi mafuta kuwa mfalme wa Israeli. 4Daudi alikuwa na miaka thelathini alipoanza kutawala, naye akatawala Israeli miaka arobaini. 5Huko Hebroni alitawala Yuda kwa miaka saba na miezi sita, na katika Yerusalemu alitawala Israeli yote na Yuda kwa miaka thelathini na mitatu. 6Mfalme na watu wake wakaenda Yerusalemu kuwashambulia Wayebusi walioishi humo. Wayebusi wakamwambia Daudi, “Wewe hutaingia humu, kwani hata vipofu na viwete wanaweza kukufukuza.” Walidhani, “Daudi hawezi kuingia humu.” 7Hata hivyo, Daudi akaiteka ngome ya Sayuni, Mji wa Daudi. 8Siku ile, Daudi akasema, “Yeyote ambaye atawashinda Wayebusi, atatumia huo mfereji kuwafikia hao ‘viwete na vipofu’ ambao ni adui za Daudi.” Ndiyo sababu wanasema, “‘Vipofu na viwete’ hawataingia kwenye jumba la ufalme.” 9Ndipo Daudi akafanya makao ndani ya ngome na kuiita Mji wa Daudi. Akajenga eneo linalozunguka kuanzia Milo kuelekea ndani. 10Daudi akazidi kuwa na nguvu zaidi na zaidi, kwa sababu Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote alikuwa pamoja naye. 11Basi Hiramu mfalme wa Tiro akawatuma wajumbe kwa Daudi, wakiwa na magogo ya mierezi, maseremala na waashi, nao wakajenga jumba la kifalme kwa ajili ya Daudi. 12Naye Daudi akafahamu kuwa Bwana amemwimarisha kuwa mfalme juu ya Israeli na ameinua ufalme wake kwa ajili ya Israeli, watu wake. 13Baada ya Daudi kuondoka Hebroni, akajitwalia masuria zaidi na wake huko Yerusalemu, nao wana na binti wengi walizaliwa kwake. 14Haya ndiyo majina ya watoto waliozaliwa kwake huko: Shamua, Shobabu, Nathani, Solomoni, 15Ibihari, Elishua, Nefegi, Yafia, 16Elishama, Eliada na Elifeleti. 17Wafilisti waliposikia kuwa Daudi ametiwa mafuta kuwa mfalme wa Israeli, wakapanda na jeshi lao lote kwenda kumsaka, lakini Daudi akapata habari hizo, naye akateremka kwenye ngome. 18Basi Wafilisti walikuwa wamekuja na kusambaa kwenye Bonde la Warefai, 19kwa hiyo Daudi akamuuliza Bwana, “Je, niende kuwashambulia Wafilisti? Je, utawatia mikononi mwangu?” Bwana akamjibu, “Nenda, kwa maana hakika nitawatia Wafilisti mikononi mwako.” 20Ndipo Daudi akaenda mpaka Baal-Perasimu, na huko akawashinda Wafilisti. Akasema, “Kama mafuriko yafurikavyo, Bwana amewafurikia adui zangu mbele yangu.” Kwa hiyo mahali hapo pakaitwa Baal-Perasimu. 21Wafilisti wakaiacha miungu yao huko, naye Daudi na watu wake wakaichukua. 22Wafilisti walikwea kwa mara nyingine na kusambaa katika Bonde la Warefai. 23Kwa hiyo Daudi akamuuliza Bwana, naye akamjibu, “Usipande moja kwa moja, bali wazungukie kwa nyuma na uwashambulie mbele ya miti ya miforosadi. 24Mara utakaposikia sauti ya kutembea kutoka kwenye vilele vya miti ya miforosadi, nenda haraka, kwa sababu hiyo itamaanisha kuwa Bwana ametangulia mbele yako kupiga jeshi la Wafilisti.” 25Basi Daudi akafanya kama Bwana alivyomwagiza, naye akawaangusha Wafilisti njia yote kuanzia Geba hadi Gezeri.
1Then came all the tribes of Israel to David to Hebron, and spoke, saying, “Behold, we are your bone and your flesh. 2In times past, when Saul was king over us, it was you who led out and brought in Israel. Yahweh said to you, ‘You shall be shepherd of my people Israel, and you shall be prince over Israel.’” 3So all the elders of Israel came to the king to Hebron; and king David made a covenant with them in Hebron before Yahweh; and they anointed David king over Israel. 4David was thirty years old when he began to reign, and he reigned forty years. 5In Hebron he reigned over Judah seven years and six months; and in Jerusalem he reigned thirty-three years over all Israel and Judah. 6The king and his men went to Jerusalem against the Jebusites, the inhabitants of the land, who spoke to David, saying, “Unless you take away the blind and the lame, you shall not come in here”; thinking, “David can’t come in here.” 7Nevertheless David took the stronghold of Zion; the same is the city of David. 8David said on that day, “Whoever strikes the Jebusites, let him get up to the watercourse, and strike the lame and the blind, who are hated by David’s soul.” Therefore they say, “The blind and the lame can’t come into the house.” 9David lived in the stronghold, and called it the city of David. David built around from Millo and inward. 10David grew greater and greater; for Yahweh, the God of Armies, was with him. 11Hiram king of Tyre sent messengers to David, and cedar trees, and carpenters, and masons; and they built David a house. 12David perceived that Yahweh had established him king over Israel, and that he had exalted his kingdom for his people Israel’s sake. 13David took him more concubines and wives out of Jerusalem, after he had come from Hebron; and there were yet sons and daughters born to David. 14These are the names of those who were born to him in Jerusalem: Shammua, and Shobab, and Nathan, and Solomon, 15and Ibhar, and Elishua, and Nepheg, and Japhia, 16and Elishama, and Eliada, and Eliphelet. 17When the Philistines heard that they had anointed David king over Israel, all the Philistines went up to seek David; and David heard of it, and went down to the stronghold. 18Now the Philistines had come and spread themselves in the valley of Rephaim. 19David inquired of Yahweh, saying, “Shall I go up against the Philistines? Will you deliver them into my hand?” Yahweh said to David, “Go up; for I will certainly deliver the Philistines into your hand.” 20David came to Baal Perazim, and David struck them there; and he said, “Yahweh has broken my enemies before me, like the breach of waters.” Therefore he called the name of that place Baal Perazim. 21They left their images there; and David and his men took them away. 22The Philistines came up yet again, and spread themselves in the valley of Rephaim. 23When David inquired of Yahweh, he said, “You shall not go up. Circle around behind them, and attack them over against the mulberry trees. 24It shall be, when you hear the sound of marching in the tops of the mulberry trees, that then you shall stir yourself up; for then Yahweh has gone out before you to strike the army of the Philistines.” 25David did so, as Yahweh commanded him, and struck the Philistines from Geba until you come to Gezer.
1Toen kwamen alle stammen van Israel tot David te Hebron; en zij spraken, zeggende: Zie, wij, uw gebeente en uw vlees zijn wij. 2Daartoe ook te voren, toen Saul koning over ons was, waart gij Israel uitvoerende en inbrengende; ook heeft de HEERE tot u gezegd: Gij zult Mijn volk Israel weiden, en gij zult tot een voorganger zijn over Israel. 3Alzo kwamen alle oudsten van Israel tot den koning te Hebron; en de koning David maakte een verbond met hen te Hebron, voor het aangezicht des HEEREN; en zij zalfden David tot koning over Israel. 4Dertig jaar was David oud, als hij koning werd; veertig jaren heeft hij geregeerd. 5Te Hebron regeerde hij over Juda zeven jaren en zes maanden; en te Jeruzalem regeerde hij drie en dertig jaren over gans Israel en Juda. 6En de koning toog met zijn mannen naar Jeruzalem, tegen de Jebusieten, die in dat land woonden. En zij spraken tot David, zeggende: Gij zult hier niet inkomen, maar de blinden en kreupelen zullen u afdrijven; dat is te zeggen: David zal hier niet inkomen. 7Maar David nam den burg Sion in; dezelve is de stad Davids. 8Want David zeide ten zelven dage: Al wie de Jebusieten slaat, en geraakt aan die watergoot, en die kreupelen, en die blinden, die van Davids ziel gehaat zijn, die zal tot een hoofd en tot een overste zijn; daarom zegt men: Een blinde en kreupele zal in het huis niet komen. 9Alzo woonde David in den burg en noemde dien Davids stad. En David bouwde rondom van Millo af en binnenwaarts. 10David nu ging geduriglijk voort, en werd groot; want de HEERE, de God der heirscharen, was met hem. 11En Hiram, de koning van Tyrus, zond boden tot David, en cederenhout, en timmerlieden, en metselaars; en zij bouwden David een huis. 12En David merkte, dat de HEERE hem tot een koning over Israel bevestigd had, en dat Hij zijn koninkrijk verheven had, om Zijns volks Israels wil. 13En David nam meer bijwijven, en vrouwen van Jeruzalem, nadat hij van Hebron gekomen was; en David werden meer zonen en dochteren geboren. 14En dit zijn de namen dergenen, die hem te Jeruzalem geboren zijn: Schammua, en Schobab, en Nathan, en Salomo. 15En Ibchar, en Elischua en Nefeg, en Jafia, 16En Elischama, en Eljade, en Elifeleth. 17Als nu de Filistijnen hoorden, dat zij David ten koning over Israel gezalfd hadden, zo togen alle Filistijnen op om David te zoeken; en David, dat horende, toog af, naar den burg. 18En de Filistijnen kwamen en verspreidden zich in het dal Refaim. 19Zo vraagde David den HEERE, zeggende: Zal ik optrekken tegen de Filistijnen? Zult Gij ze in mijn hand geven? En de HEERE zeide tot David: Trek op, want Ik zal de Filistijnen zekerlijk in uw hand geven. 20Toen kwam David te Baal-Perazim; en David sloeg hen aldaar, en zeide: De HEERE heeft mijn vijanden voor mijn aangezicht gescheurd, als een scheur der wateren; daarom noemde hij den naam derzelve plaats, Baal-Perazim. 21En zij lieten hun afgoden aldaar; en David en zijn mannen namen ze op. 22Daarna togen de Filistijnen weder op; en zij verspreidden zich in het dal Refaim. 23En David vraagde den HEERE, Dewelke zeide: Gij zult niet optrekken; maar trek om tot achter hen, dat gij aan hen komt van tegenover de moerbezienbomen; 24En het geschiede, als gij hoort het geruis van een gang in de toppen der moerbezienbomen, dan rep u; want alsdan is de HEERE voor uw aangezicht uitgegaan, om het heirleger der Filistijnen te slaan. 25En David deed alzo, gelijk als de HEERE hem geboden had; en hij sloeg de Filistijnen van Geba af, totdat gij komt te Gezer.
Bonyeza Enter ili kuuwekea mstari huu rangi, kuandika maelezo au kuunakili. Vitufe vya mishale vinakupeleka kwenye mstari unaofuata.
Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.