1Daudi alimwimbia Bwana maneno ya wimbo huu wakati Bwana alipomwokoa mikononi mwa adui zake wote, na pia mkononi mwa Sauli. 2Akasema: “Bwana ni mwamba wangu, ngome yangu na mwokozi wangu, 3Mungu wangu ni mwamba wangu, ambaye kwake ninakimbilia, ngao yangu na pembe ya wokovu wangu. Yeye ni ngome yangu, kimbilio langu na mwokozi wangu, huniokoa kutoka kwa watu wenye jeuri. 4Ninamwita Bwana, anayestahili kusifiwa, nami ninaokolewa kutoka kwa adui zangu. 5“Mawimbi ya mauti yalinizunguka, mafuriko ya maangamizi yalinilemea. 6Kamba za kuzimu zilinizunguka, mitego ya mauti ilinikabili. 7Katika shida yangu nalimwita Bwana, nilimlilia Mungu wangu. Kutoka Hekaluni mwake alisikia sauti yangu, kilio changu kikafika masikioni mwake. 8“Dunia ilitetemeka na kutikisika, misingi ya mbingu ikatikisika, vilitetemeka kwa sababu alikuwa amekasirika. 9Moshi ukapanda kutoka puani mwake, moto uteketezao ukatoka kinywani mwake, makaa ya moto yawakayo yakatoka ndani mwake. 10Akazipasua mbingu akashuka chini, mawingu meusi yalikuwa chini ya miguu yake. 11Alipanda juu ya kerubi akaruka, akapaa juu kwa mbawa za upepo. 12Alifanya giza hema lake la kujifunika: mawingu meusi ya mvua ya angani. 13Kutokana na mwanga wa uwepo wake mawingu yalisogea, ikanyesha mvua ya mawe na umeme wa radi. 14Bwana alinguruma kutoka mbinguni, sauti ya Aliye Juu Sana ilisikika. 15Aliipiga mishale na kutawanya adui, umeme wa radi na kuwafukuza. 16Mabonde ya bahari yalifunuliwa, na misingi ya dunia ikawa wazi kwa kukaripia kwake Bwana, kwa uvumi wa pumzi kutoka puani mwake. 17“Alinyoosha mkono kutoka juu na kunishika; alinitoa kutoka kilindi cha maji makuu. 18Aliniokoa kutoka adui wangu mwenye nguvu nyingi, kutoka adui zangu waliokuwa na nguvu nyingi kuliko mimi. 19Walinikabili siku ya msiba wangu, lakini Bwana alikuwa msaada wangu. 20Alinileta nje mahali penye nafasi tele, akaniokoa kwa kuwa alipendezwa nami. 21“Bwana alinitendea sawasawa na uadilifu wangu; sawasawa na usafi wa mikono yangu amenilipa. 22Kwa maana nimezishika njia za Bwana; sijatenda ubaya nikamwacha Mungu wangu. 23Sheria zake zote zi mbele yangu, wala sijayaacha maagizo yake. 24Nimekuwa sina hatia mbele zake, nami nimejilinda nisitende dhambi. 25Bwana amenilipa sawasawa na uadilifu wangu, sawasawa na usafi wangu machoni pake. 26“Kwa yeye aliye mwaminifu unajionyesha kuwa mwaminifu, kwa asiye na hatia unajionyesha kutokuwa na hatia, 27kwa aliye mtakatifu unajionyesha kuwa mtakatifu, lakini kwa aliyepotoka unajionyesha kuwa mkaidi. 28Wewe huwaokoa wanyenyekevu, lakini macho yako ni juu ya wenye kiburi ili uwashushe. 29Wewe ni taa yangu, Ee Bwana. Bwana hulifanya giza langu kuwa mwanga. 30Kwa msaada wako naweza kushinda jeshi, nikiwa pamoja na Mungu wangu nitaweza kuruka ukuta. 31“Kuhusu Mungu, njia yake ni kamilifu; neno la Bwana halina dosari. Yeye ni ngao kwa wote wanaokimbilia kwake. 32Kwa maana ni nani aliye Mungu zaidi ya Bwana? Ni nani aliye Mwamba isipokuwa Mungu wetu? 33Mungu ndiye anivikaye nguvu na kufanya njia yangu kuwa kamilifu. 34Huifanya miguu yangu kama miguu ya kulungu, huniwezesha kusimama mahali palipo juu. 35Huifundisha mikono yangu kupigana vita; mikono yangu inaweza kupinda upinde wa shaba. 36Hunipa ngao yako ya ushindi, unajishusha chini ili kuniinua. 37Huyapanua mapito yangu, ili miguu yangu isiteleze. 38“Niliwafuatia adui zangu na nikawaseta, sikurudi nyuma mpaka walipoangamizwa. 39Niliwaseta kabisa, nao hawakuweza kuinuka tena; walianguka chini ya miguu yangu. 40Ulinivika nguvu kwa ajili ya kupigana vita; uliwafanya adui zangu wasujudu miguuni pangu. 41Uliwafanya adui zangu wageuke na kukimbia, nami nikawaangamiza adui zangu. 42Walipiga yowe, lakini hapakuwepo na yeyote wa kuwaokoa; walimlilia Bwana, lakini hakuwajibu. 43Niliwaponda kama mavumbi ya nchi; niliwaponda na kuwakanyaga kama tope barabarani. 44“Umeniokoa kutokana na mashambulizi ya watu wangu; umenihifadhi mimi kama kiongozi wa mataifa. Watu ambao sikuwajua wananitumikia, 45nao wageni huja wakininyenyekea, mara wanisikiapo, hunitii. 46Wote wanalegea, wanatoka katika ngome zao wakitetemeka. 47“Bwana yu hai! Sifa ni kwa Mwamba wangu! Atukuzwe Mungu, Mwamba, Mwokozi wangu! 48Yeye ndiye Mungu anilipiziaye kisasi, ayawekaye mataifa chini yangu, 49aniwekaye huru toka kwa adui zangu. Uliniinua juu ya adui zangu; uliniokoa toka kwa watu wajeuri. 50Kwa hiyo nitakusifu, Ee Bwana, katikati ya mataifa; nitaliimbia sifa jina lako. 51Humpa mfalme wake ushindi mkuu; huonyesha fadhili zake kwa mpakwa mafuta wake, kwa Daudi na wazao wake milele.”
1David spoke to Yahweh the words of this song in the day that Yahweh delivered him out of the hand of all his enemies, and out of the hand of Saul: 2and he said, “Yahweh is my rock, my fortress, and my deliverer, even mine; 3God, my rock, in him I will take refuge; my shield, and the horn of my salvation, my high tower, and my refuge. My savior, you save me from violence. 4I will call on Yahweh, who is worthy to be praised: So shall I be saved from my enemies. 5For the waves of death surrounded me. The floods of ungodliness made me afraid. 6The cords of Sheol were around me. The snares of death caught me. 7In my distress I called on Yahweh. Yes, I called to my God. He heard my voice out of his temple. My cry came into his ears. 8Then the earth shook and trembled. The foundations of heaven quaked and were shaken, because he was angry. 9Smoke went up out of his nostrils. Fire out of his mouth devoured. Coals were kindled by it. 10He bowed the heavens also, and came down. Thick darkness was under his feet. 11He rode on a cherub, and flew. Yes, he was seen on the wings of the wind. 12He made darkness pavilions around himself: gathering of waters, and thick clouds of the skies. 13At the brightness before him, coals of fire were kindled. 14Yahweh thundered from heaven. The Most High uttered his voice. 15He sent out arrows, and scattered them; lightning, and confused them. 16Then the channels of the sea appeared. The foundations of the world were laid bare by the rebuke of Yahweh, At the blast of the breath of his nostrils. 17He sent from on high and he took me. He drew me out of many waters. 18He delivered me from my strong enemy, from those who hated me, for they were too mighty for me. 19They came on me in the day of my calamity, but Yahweh was my support. 20He also brought me out into a large place. He delivered me, because he delighted in me. 21Yahweh rewarded me according to my righteousness. He rewarded me according to the cleanness of my hands. 22For I have kept the ways of Yahweh, and have not wickedly departed from my God. 23For all his ordinances were before me. As for his statutes, I did not depart from them. 24I was also perfect toward him. I kept myself from my iniquity. 25Therefore Yahweh has rewarded me according to my righteousness, According to my cleanness in his eyesight. 26With the merciful you will show yourself merciful. With the perfect man you will show yourself perfect. 27With the pure you will show yourself pure. With the crooked you will show yourself shrewd. 28You will save the afflicted people, But your eyes are on the haughty, that you may bring them down. 29For you are my lamp, Yahweh. Yahweh will light up my darkness. 30For by you, I run against a troop. By my God, I leap over a wall. 31As for God, his way is perfect. Yahweh’s word is tested. He is a shield to all those who take refuge in him. 32For who is God, besides Yahweh? Who is a rock, besides our God? 33God is my strong fortress. He makes my way perfect. 34He makes his feet like hinds’ feet, and sets me on my high places. 35He teaches my hands to war, so that my arms bend a bow of brass. 36You have also given me the shield of your salvation. Your gentleness has made me great. 37You have enlarged my steps under me. My feet have not slipped. 38I have pursued my enemies and destroyed them. I didn’t turn again until they were consumed. 39I have consumed them, and struck them through, so that they can’t arise. Yes, they have fallen under my feet. 40For you have armed me with strength for the battle. You have subdued under me those who rose up against me. 41You have also made my enemies turn their backs to me, that I might cut off those who hate me. 42They looked, but there was no one to save; even to Yahweh, but he didn’t answer them. 43Then I beat them as small as the dust of the earth. I crushed them as the mire of the streets, and spread them abroad. 44You also have delivered me from the strivings of my people. You have kept me to be the head of the nations. A people whom I have not known will serve me. 45The foreigners will submit themselves to me. As soon as they hear of me, they will obey me. 46The foreigners will fade away, and will come trembling out of their close places. 47Yahweh lives! Blessed be my rock! Exalted be God, the rock of my salvation, 48even the God who executes vengeance for me, who brings down peoples under me, 49who brings me away from my enemies. Yes, you lift me up above those who rise up against me. You deliver me from the violent man. 50Therefore I will give thanks to you, Yahweh, among the nations, and will sing praises to your name. 51He gives great deliverance to his king, and shows loving kindness to his anointed, to David and to his seed, forever more.”
1En David sprak de woorden dezes lieds tot den HEERE, ten dage als de HEERE hem verlost had uit de hand van al zijn vijanden, en uit de hand van Saul. 2Hij zeide dan: De HEERE is mij mijn Steenrots, en mijn Burg, en mijn Uithelper. 3God is mijn Rots, ik zal op Hem betrouwen; mijn Schild en de Hoorn mijns heils, mijn Hoog Vertrek en mijn Toevlucht, mijn Verlosser! Van geweld hebt Gij mij verlost! 4Ik riep den HEERE aan, Die te prijzen is, en ik werd verlost van mijn vijanden. 5Want baren des doods hadden mij omvangen; beken Belials verschrikten mij. 6Banden der hel omringden mij; strikken des doods bejegenden mij. 7Als mij bange was, riep ik den HEERE aan, en riep tot mijn God; en Hij hoorde mijn stem uit Zijn paleis, en mijn geroep kwam in Zijn oren. 8Toen daverde en beefde de aarde; de fondamenten des hemels beroerden zich, en daverden, omdat Hij ontstoken was. 9Rook ging op van Zijn neus, en een vuur uit Zijn mond verteerde; kolen werden daarvan aangestoken. 10En Hij boog den hemel, en daalde neder; en donkerheid was onder Zijn voeten. 11En Hij voer op een cherub, en vloog, en werd gezien op de vleugelen des winds. 12En Hij zette duisternis rondom Zich tot tenten, een samenbinding der wateren, wolken des hemels. 13Van den glans voor Hem henen werden kolen des vuurs aangestoken. 14De HEERE donderde van den hemel, en de Allerhoogste gaf Zijn stem. 15En Hij zond pijlen uit en verstrooide ze; bliksemen en verschrikte ze. 16En de diepe kolken der zee werden gezien, de gronden der wereld werden ontdekt, door het schelden des HEEREN, van het geblaas des winds van Zijn neus. 17Hij zond van de hoogte, Hij nam mij, Hij trok mij op uit grote wateren. 18Hij verloste mij van mijn sterken vijand, van mijn haters, omdat zij machtiger waren dan ik. 19Zij hadden mij bejegend ten dage mijns ongevals; maar de HEERE was mij een Steunsel. 20En Hij voerde mij uit in de ruimte, en rukte mij uit, want Hij had lust aan mij. 21De HEERE vergold mij naar mijn gerechtigheid; Hij gaf mij weder naar de reinigheid mijner handen. 22Want ik heb des HEEREN wegen gehouden, en ben van mijn God niet goddelooslijk afgegaan. 23Want al Zijn rechten waren voor mij, en Zijn inzettingen, daarvan week ik niet af. 24Maar ik was oprecht voor Hem; en ik wachtte mij voor mijn ongerechtigheid. 25Zo gaf mij de HEERE weder naar mijn gerechtigheid, naar mijn reinigheid, voor Zijn ogen. 26Bij den goedertierene houdt Gij U goedertieren; bij den oprechten held houdt Gij U oprecht. 27Bij den reine houdt Gij U rein; maar bij den verkeerde houdt Gij U verdraaid. 28En Gij verlost het bedrukte volk; maar Uw ogen zijn tegen de hogen, Gij zult hen vernederen. 29Want Gij zijt mijn Lamp, o HEERE, en de HEERE doet mijn duisternis opklaren. 30Want met U loop ik door een bende; met mijn God spring ik over een muur. 31Gods weg is volmaakt; de rede des HEEREN is doorlouterd; Hij is een Schild allen, die op Hem betrouwen. 32Want wie is God, behalve de HEERE, en wie is een rotssteen, behalve onze God? 33God is mijn Sterkte en Kracht; en Hij heeft mijn weg volkomen geopend. 34Hij maakt mijn voeten gelijk als der hinden, en stelt mij op mijn hoogten. 35Hij leert mijn handen ten strijde, zodat een stalen boog met mijn armen verbroken is. 36Ook hebt Gij mij gegeven het schild Uws heils, en door Uw verootmoedigen hebt Gij mij groot gemaakt. 37Gij hebt mijn voetstap ruim gemaakt onder mij; en mijn enkelen hebben niet gewankeld. 38Ik vervolgde mijn vijanden, en verdelgde hen, en keerde niet weder, totdat ik ze verdaan had. 39En ik verteerde hen, en doorstak ze, dat zij niet weder opstonden; maar zij vielen onder mijn voeten. 40Want Gij omgorddet mij met kracht ten strijde; Gij deedt onder mij nederbukken, die tegen mij opstonden. 41En Gij gaaft mij den nek mijner vijanden, mijner haters, en ik vernielde hen. 42Zij zagen uit, maar er was geen verlosser; naar den HEERE, maar Hij antwoordde hun niet. 43Toen vergruisde ik hen als stof der aarde; ik stampte ze, ik breidde hen uit als slijk der straten. 44Ook hebt Gij mij uitgeholpen van de twisten mijns volks, Gij hebt mij bewaard tot een hoofd der heidenen; het volk, dat ik niet kende, heeft mij gediend. 45Vreemden hebben zich mij geveinsdelijk onderworpen; zo haast als hun oor van mij hoorde, hebben zij mij gehoorzaamd. 46Vreemden zijn vervallen, en hebben zich aangegord uit hun sloten. 47De HEERE leeft, en geloofd zij mijn Rotssteen; en verhoogd zij God, de Rotssteen mijns heils! 48De God, Die mij volkomene wraak geeft, en de volken onder mij nederwerpt; 49En Die mij uitvoert van mijn vijanden; en Gij verhoogt mij boven degenen, die tegen mij opstaan; Gij redt mij van den man alles gewelds. 50Daarom zal ik U, o HEERE, loven onder de heidenen, en Uw Naam zal ik psalmzingen. 51Hij is een Toren der verlossingen Zijns konings, en Hij doet goedertierenheid aan Zijn gezalfde, aan David en aan zijn zaad, tot in eeuwigheid.
Bonyeza Enter ili kuuwekea mstari huu rangi, kuandika maelezo au kuunakili. Vitufe vya mishale vinakupeleka kwenye mstari unaofuata.
Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.