1Ikawa Rehoboamu alipofika Yerusalemu, akakusanya nyumba ya Yuda na ya Benyamini, wanaume wapiganaji 180,000, kufanya vita dhidi ya nyumba ya Israeli na kuurudisha tena ufalme kwa Rehoboamu mwana wa Solomoni. 2Lakini neno hili la Bwana likamjia Shemaya mtu wa Mungu: 3“Mwambie Rehoboamu mwana wa Solomoni mfalme wa Yuda, na Israeli wote walioko Yuda na Benyamini, 4‘Hili ndilo asemalo Bwana: Msipande kupigana dhidi ya ndugu zenu. Nendeni nyumbani, kila mmoja wenu, kwa kuwa hili nimelitenda mimi.’” Kwa hiyo wakalitii neno la Bwana na wakaacha kwenda kupigana dhidi ya Yeroboamu. 5Rehoboamu akaishi Yerusalemu akajenga miji yenye ngome katika Yuda: 6Akajenga Bethlehemu, Etamu, Tekoa, 7Beth-Suri, Soko, Adulamu, 8Gathi, Maresha, Zifu, 9Adoraimu, Lakishi, Azeka, 10Sora, Aiyaloni na Hebroni. Hii ndiyo iliyokuwa miji iliyojengewa ngome katika Yuda na Benyamini. 11Akaimarisha ulinzi wake na kuweka majemadari ndani yake, pamoja na ghala za mahitaji ya vyakula, mafuta ya zeituni na divai. 12Akaweka ngao na mikuki katika miji na kuifanya iwe imara sana. Kwa hiyo Yuda na Benyamini zikawa zake. 13Makuhani na Walawi kutoka sehemu zote za Israeli wakawa upande wake. 14Pia Walawi wakaacha maeneo yao ya malisho na mali zao, wakaja Yuda na Yerusalemu kwa sababu Yeroboamu na wanawe walikuwa wamewakataa wasiwe makuhani wa Bwana. 15Naye akawa amechagua makuhani wake mwenyewe kwa ajili ya mahali pa juu pa kuabudia sanamu za mbuzi na za ndama ambazo alikuwa ametengeneza. 16Wale waliotoka katika kila kabila la Israeli ambao walielekeza mioyo yao kumtafuta Bwana, Mungu wa Israeli, wakawafuata Walawi huko Yerusalemu kumtolea Bwana dhabihu, Mungu wa baba zao. 17Wakaimarisha ufalme wa Yuda na kumuunga mkono Rehoboamu mwana wa Solomoni miaka mitatu, wakienenda katika njia za Daudi na Solomoni katika wakati huu. 18Rehoboamu alimwoa Mahalati ambaye alikuwa binti Yeremothi mwana wa Daudi, mamaye alikuwa Abihaili binti Eliabu mwana wa Yese. 19Mahalati alimzalia Rehoboamu wana: Yeushi, Shemaria na Zahamu. 20Kisha akamwoa Maaka binti Absalomu, ambaye alimzalia: Abiya, Atai, Ziza na Shelomithi. 21Rehoboamu akampenda Maaka binti Absalomu zaidi kuliko wakeze wengine na masuria wake. Kwa jumla alikuwa na wake kumi na wanane na masuria sitini, wana ishirini na wanane na binti sitini. 22Rehoboamu akamweka Abiya mwana wa Maaka, kuwa mkuu wa wana wa mfalme miongoni mwa ndugu zake ili amfanye mfalme. 23Akatenda kwa busara, akiwasambaza baadhi ya wanawe katika wilaya zote za Yuda na Benyamini, pamoja na miji yote yenye ngome. Akawapa mahitaji tele na kuwaoza wake wengi.
1When Rehoboam had come to Jerusalem, he assembled the house of Judah and Benjamin, one hundred eighty thousand chosen men, who were warriors, to fight against Israel, to bring the kingdom again to Rehoboam. 2But Yahweh’s word came to Shemaiah the man of God, saying, 3“Speak to Rehoboam the son of Solomon, king of Judah, and to all Israel in Judah and Benjamin, saying, 4‘Thus says Yahweh, “You shall not go up, nor fight against your brothers! Return every man to his house; for this thing is of me.”’” So they listened to Yahweh’s words, and returned from going against Jeroboam. 5Rehoboam lived in Jerusalem, and built cities for defense in Judah. 6He built Bethlehem, and Etam, and Tekoa, 7Beth Zur, and Soco, and Adullam, 8and Gath, and Mareshah, and Ziph, 9and Adoraim, and Lachish, and Azekah, 10and Zorah, and Aijalon, and Hebron, which are in Judah and in Benjamin, fortified cities. 11He fortified the strongholds, and put captains in them, and stores of food, and oil and wine. 12He put shields and spears in every city, and made them exceeding strong. Judah and Benjamin belonged to him. 13The priests and the Levites who were in all Israel resorted to him out of all their border. 14For the Levites left their suburbs and their possession, and came to Judah and Jerusalem: for Jeroboam and his sons cast them off, that they should not execute the priest’s office to Yahweh; 15and he appointed him priests for the high places, and for the male goats, and for the calves which he had made. 16After them, out of all the tribes of Israel, such as set their hearts to seek Yahweh, the God of Israel, came to Jerusalem to sacrifice to Yahweh, the God of their fathers. 17So they strengthened the kingdom of Judah, and made Rehoboam the son of Solomon strong, three years; for they walked three years in the way of David and Solomon. 18Rehoboam took him a wife, Mahalath the daughter of Jerimoth the son of David, and of Abihail the daughter of Eliab the son of Jesse; 19and she bore him sons: Jeush, and Shemariah, and Zaham. 20After her he took Maacah the daughter of Absalom; and she bore him Abijah, and Attai, and Ziza, and Shelomith. 21Rehoboam loved Maacah the daughter of Absalom above all his wives and his concubines: (for he took eighteen wives, and sixty concubines, and became the father of twenty-eight sons and sixty daughters.) 22Rehoboam appointed Abijah the son of Maacah to be chief, the prince among his brothers; for he intended to make him king. 23He dealt wisely, and dispersed of all his sons throughout all the lands of Judah and Benjamin, to every fortified city: and he gave them food in abundance. He sought for them many wives.
1Toen nu Rehabeam te Jeruzalem gekomen was, vergaderde hij het huis van Juda en Benjamin, eenhonderd en tachtig duizend, uitgelezenen, geoefend ten oorlog, om tegen Israel te strijden, opdat hij het koninkrijk weder aan Rehabeam bracht. 2Doch het woord des HEEREN geschiedde tot Semaja, den man Gods, zeggende: 3Zeg tot Rehabeam, den zoon van Salomo, den koning van Juda, en tot het ganse Israel in Juda en Benjamin, zeggende: 4Zo zegt de HEERE: Gij zult niet optrekken, noch strijden tegen uw broederen; een ieder kere weder tot zijn huis, want deze zaak is van Mij geschied. En zij hoorden de woorden des HEEREN, en zij keerden weder van tegen Jerobeam te trekken. 5Rehabeam nu woonde te Jeruzalem; en hij bouwde steden tot vastigheden in Juda. 6Hij bouwde nu Bethlehem, en Etham, en Thekoa, 7En Beth-Zur, en Socho, en Adullam, 8En Gath, en Maresa, en Zif, 9En Adoraim, en Lachis, en Azeka, 10En Zora, en Ajalon, en Hebron; dewelke in Juda en in Benjamin de vaste steden waren. 11En hij sterkte deze vastigheden, en legde oversten daarin, en schatten van spijs, en olie, en wijn; 12En in elke stad rondassen en spiesen, en sterkte ze gans zeer; zo was Juda, en Benjamin zijne. 13Daartoe de priesteren en de Levieten, die in het ganse Israel waren, stelden zich bij hem uit al hun landpalen. 14Want de Levieten verlieten hun voorsteden en hun bezitting, en kwamen in Juda en in Jeruzalem; want Jerobeam en zijn zonen hadden hen verstoten, van het priesterdom des HEEREN te mogen bedienen. 15En hij had zich priesteren gesteld voor de hoogte, en voor de duivelen, en voor de kalveren, die hij gemaakt had. 16Na die kwamen ook uit alle stammen van Israel te Jeruzalem, die hun hart begaven, om den HEERE, den God Israels, te zoeken, dat zij den HEERE, den God hunner vaderen, offerande deden. 17Alzo sterkten zij het koninkrijk van Juda, en bekrachtigden Rehabeam, den zoon van Salomo, drie jaren; want drie jaren wandelden zij in den weg van David, en Salomo. 18En Rehabeam nam zich, benevens Mahalath, de dochter van Jerimoth, den zoon van David, ter vrouwe Abihail, de dochter van Eliab, den zoon van Isai, 19Dewelke hem zonen baarde, Jeus, en Semaria, en Zaham. 20En na haar nam hij Maacha, de dochter van Absalom; deze baarde hem Abia, en Attai, en Ziza, en Selomith. 21En Rehabeam had Maacha, Absaloms dochter, liever dan al zijn vrouwen en zijn bijwijven; want hij had achttien vrouwen genomen, en zestig bijwijven; en hij gewon acht en twintig zonen en zestig dochteren. 22En Rehabeam stelde Abia, den zoon van Maacha, tot een hoofd, om een overste te zijn onder zijn broederen; want het was om hem koning te maken. 23En hij handelde verstandelijk, dat hij van al zijn zonen, door alle landen van Juda en Benjamin, in alle vaste steden verspreidde, denwelken hij spijze gaf in overvloed; en hij begeerde de veelheid van vrouwen.
Bonyeza Enter ili kuuwekea mstari huu rangi, kuandika maelezo au kuunakili. Vitufe vya mishale vinakupeleka kwenye mstari unaofuata.
Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.