1Afadhali sifa nzuri kuliko manukato safi, nayo siku ya kufa kuliko ya kuzaliwa. 2Afadhali kwenda kwenye nyumba ya msiba kuliko kwenda kwenye nyumba ya karamu, kwa kuwa kifo ni hatima ya kila mwanadamu, imewapasa walio hai kuliweka hili mioyoni mwao. 3Huzuni ni afadhali kuliko kicheko, kwa sababu uso wenye huzuni wafaa kwa moyo. 4Moyo wa wenye hekima uko katika nyumba ya msiba, lakini moyo wa wapumbavu uko katika nyumba ya anasa. 5Afadhali kusikia karipio la mtu mwenye hekima, kuliko kusikiliza wimbo wa wapumbavu. 6Kama ilivyo kuvunjika kwa miiba chini ya sufuria, ndivyo kilivyo kicheko cha wapumbavu. Hili nalo pia ni ubatili. 7Dhuluma humfanya mtu mwenye hekima kuwa mpumbavu, nayo rushwa huuharibu moyo. 8Mwisho wa jambo ni bora kuliko mwanzo wake, uvumilivu ni bora kuliko kiburi. 9Usiwe mwepesi kukasirika rohoni mwako, kwa kuwa hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu. 10Usiseme, “Kwa nini siku za kale zilikuwa bora kuliko siku hizi?” Kwa maana si hekima kuuliza maswali kama hayo. 11Hekima, kama ulivyo urithi, ni kitu chema na huwafaidia wale walionalo jua. 12Hekima ni ulinzi kama fedha ilivyo ulinzi, lakini faida ya maarifa ni hii: kwamba hekima huhifadhi maisha ya aliye nayo. 13Tafakari kile Mungu alichokitenda: Nani awezaye kunyoosha kile ambacho yeye amekipinda? 14Nyakati zikiwa nzuri, ufurahi, lakini nyakati zikiwa mbaya, tafakari: Mungu amefanya hiyo moja, naam, sanjari na hiyo nyingine. Kwa hiyo, mwanadamu hawezi kugundua kitu chochote kuhusu maisha yake ya baadaye. 15Katika maisha haya yangu ya ubatili nimeshaona haya mawili: mtu mwadilifu akiangamia katika uadilifu wake, naye mtu mwovu akiishi maisha marefu katika uovu wake. 16Usiwe mwenye haki kupita kiasi, wala usiwe na hekima kupita kiasi: kwa nini kujiangamiza mwenyewe? 17Usiwe mwovu kupita kiasi, wala usiwe mpumbavu: kwa nini kufa kabla ya wakati wako? 18Ni vyema kushika hilo moja na wala usiache hilo jingine likupite. Mtu amchaye Mungu ataepuka huko kupita kiasi. 19Hekima humfanya yeye aliye nayo kuwa na uwezo zaidi kuliko watawala kumi katika mji. 20Hakuna mtu mwenye haki duniani ambaye hufanya mambo ya haki na kamwe asitende dhambi. 21Usitie maanani kila neno linalosemwa na watu, la sivyo, waweza kumsikia mtumishi wako akikulaani: 22kwa kuwa unafahamu moyoni mwako kwamba wewe mwenyewe mara nyingi umewalaani wengine. 23Yote haya niliyajaribu kwa hekima, nikasema, “Nimeamua kuwa na hekima”: lakini hii ilikuwa nje ya uwezo wangu. 24Vyovyote hekima ilivyo, hekima iko mbali sana na imejificha, ni nani awezaye kuigundua? 25Nikageuza fikira zangu ili kuelewa, kuchunguza na kuitafuta hekima na kusudi la mambo, na ili kuelewa ujinga wa uovu, na wazimu wa upumbavu. 26Nimeona jambo lililo chungu kuliko mauti, mwanamke ambaye ni mtego, ambaye moyo wake ni wavu wa kutegea na mikono yake ni minyororo. Mtu ampendezaye Mungu atamkwepa, bali mwenye dhambi atanaswa naye. 27Mhubiri anasema, “Tazama, hili ndilo nililogundua: “Nimegundua kitu kimoja baada ya kingine nilipokuwa katika kusudi la mambo: 28ningali natafiti lakini sipati: nilimpata mwanaume mmoja mnyofu miongoni mwa elfu, lakini hakuna mwanamke mmoja mnyofu miongoni mwao. 29Hili ndilo peke yake nililolipata: Mungu amemuumba mwanadamu mnyofu, lakini mwanadamu amebuni mambo mengi.”
1A good name is better than fine perfume; and the day of death better than the day of one’s birth. 2It is better to go to the house of mourning than to go to the house of feasting: for that is the end of all men, and the living should take this to heart. 3Sorrow is better than laughter; for by the sadness of the face the heart is made good. 4The heart of the wise is in the house of mourning; but the heart of fools is in the house of mirth. 5It is better to hear the rebuke of the wise, than for a man to hear the song of fools. 6For as the crackling of thorns under a pot, so is the laughter of the fool. This also is vanity. 7Surely extortion makes the wise man foolish; and a bribe destroys the understanding. 8Better is the end of a thing than its beginning. The patient in spirit is better than the proud in spirit. 9Don’t be hasty in your spirit to be angry, for anger rests in the bosom of fools. 10Don’t say, “Why were the former days better than these?” For you do not ask wisely about this. 11Wisdom is as good as an inheritance. Yes, it is more excellent for those who see the sun. 12For wisdom is a defense, even as money is a defense; but the excellency of knowledge is that wisdom preserves the life of him who has it. 13Consider the work of God, for who can make that straight, which he has made crooked? 14In the day of prosperity be joyful, and in the day of adversity consider; yes, God has made the one side by side with the other, to the end that man should not find out anything after him. 15All this have I seen in my days of vanity: there is a righteous man who perishes in his righteousness, and there is a wicked man who lives long in his evildoing. 16Don’t be overly righteous, neither make yourself overly wise. Why should you destroy yourself? 17Don’t be too wicked, neither be foolish. Why should you die before your time? 18It is good that you should take hold of this. Yes, also from that don’t withdraw your hand; for he who fears God will come out of them all. 19Wisdom is a strength to the wise man more than ten rulers who are in a city. 20Surely there is not a righteous man on earth, who does good and doesn’t sin. 21Also don’t take heed to all words that are spoken, lest you hear your servant curse you; 22for often your own heart knows that you yourself have likewise cursed others. 23All this have I proved in wisdom. I said, “I will be wise”; but it was far from me. 24That which is, is far off and exceedingly deep. Who can find it out? 25I turned around, and my heart sought to know and to search out, and to seek wisdom and the scheme of things, and to know that wickedness is stupidity, and that foolishness is madness. 26I find more bitter than death the woman whose heart is snares and traps, whose hands are chains. Whoever pleases God shall escape from her; but the sinner will be ensnared by her. 27“Behold, I have found this,” says the Preacher, “one to another, to find out the scheme; 28which my soul still seeks; but I have not found. One man among a thousand have I found; but I have not found a woman among all those. 29Behold, this only have I found: that God made man upright; but they search for many schemes.”
1Beter is een goede naam, dan goede olie, en de dag des doods, dan de dag dat iemand geboren wordt. 2Het is beter te gaan in het klaaghuis, dan te gaan in het huis des maaltijds; want in hetzelve is het einde aller mensen, en de levende legt het in zijn hart. 3Het treuren is beter dan het lachen; want door de droefheid des aangezichts wordt het hart gebeterd. 4Het hart der wijzen is in het klaaghuis; maar het hart der zotten in het huis der vreugde. 5Het is beter te horen het bestraffen des wijzen, dan dat iemand hore het gezang der dwazen. 6Want gelijk het geluid der doornen onder een pot is, alzo is het lachen eens zots. Dit is ook ijdelheid. 7Voorwaar, de onderdrukking zou wel een wijze dol maken; en het geschenk verderft het hart. 8Het einde van een ding is beter dan zijn begin; de lankmoedige is beter dan de hoogmoedige. 9Zijt niet haastig in uw geest om te toornen; want de toorn rust in den boezem der dwazen. 10Zeg niet: Wat is er, dat de vorige dagen beter geweest zijn, dan deze? Want gij zoudt naar zulks niet uit wijsheid vragen. 11De wijsheid is goed met een erfdeel; en degenen, die de zon aanschouwen, hebben voordeel daarvan. 12Want de wijsheid is tot een schaduw, en het geld is tot een schaduw; maar de uitnemendheid der wetenschap is, dat de wijsheid haar bezitters het leven geeft. 13Aanmerk het werk Gods; want wie kan recht maken, dat Hij krom gemaakt heeft? 14Geniet het goede ten dage des voorspoeds, maar ten dage des tegenspoeds, zie toe; want God maakt ook den een tegenover den ander, ter oorzake dat de mens niet zou vinden iets, dat na hem zal zijn. 15Dit alles heb ik gezien in de dagen mijner ijdelheid; er is een rechtvaardige, die in zijn gerechtigheid omkomt; daarentegen is er een goddeloze, die in zijn boosheid zijn dagen verlengt. 16Wees niet al te rechtvaardig, noch houd uzelven al te wijs; waarom zoudt gij verwoesting over u brengen? 17Wees niet al te goddeloos, noch wees al te dwaas; waarom zoudt gij sterven buiten uw tijd? 18Het is goed, dat gij daaraan vasthoudt, en trek ook uw hand van dit niet af; want die God vreest, dien ontgaat dat al. 19De wijsheid versterkt den wijze meer dan tien heerschappers, die in een stad zijn. 20Voorwaar, er is geen mens rechtvaardig op aarde, die goed doet, en niet zondigt. 21Geef ook uw hart niet tot alle woorden, die men spreekt, opdat gij niet hoort, dat uw knecht u vloekt. 22Want uw hart heeft ook veelmalen bekend, dat gij ook anderen gevloekt hebt. 23Dit alles heb ik met wijsheid verzocht; ik zeide: Ik zal wijsheid bekomen, maar zij was nog verre van mij. 24Hetgeen verre af is, en zeer diep, wie zal dat vinden? 25Ik keerde mij om, en mijn hart, om te weten, en om na te sporen, en te zoeken wijsheid en een sluitrede; en om te weten de goddeloosheid der zotheid, en de dwaasheid der onzinnigheden. 26En ik vond een bitterder ding, dan de dood: een vrouw, welker hart netten en garen, en haar handen banden zijn; wie goed is voor Gods aangezicht, zal van haar ontkomen; daarentegen de zondaar zal van haar gevangen worden. 27Ziet, dit heb ik gevonden, zegt de prediker, het ene bij het andere, om de sluitrede te vinden; 28Dewelke mijn ziel nog zoekt, maar ik heb haar niet gevonden: een man uit duizend heb ik gevonden; maar een vrouw onder die allen heb ik niet gevonden. 29Alleenlijk ziet, dit heb ik gevonden, dat God den mens recht gemaakt heeft, maar zij hebben veel vonden gezocht.
Bonyeza Enter ili kuuwekea mstari huu rangi, kuandika maelezo au kuunakili. Vitufe vya mishale vinakupeleka kwenye mstari unaofuata.
Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.