Ruka hadi kwenye maudhui
Beta
Mwonekano

Uzi bado haujatafsiriwa kikamilifu kwa Kiswahili. Kile ambacho bado hakijatafsiriwa kinaonyeshwa kwa Kiingereza.

Malaki 4

Sura hii ni sehemu ya: De bode en de dag

1“Hakika siku inakuja, itawaka kama tanuru. Wote wenye kiburi na kila mtenda mabaya watakuwa mabua makavu, na siku ile inayokuja itawawasha moto,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote. “Hakuna mzizi wala tawi litakalosalia kwao. 2Bali kwenu ninyi mnaoliheshimu Jina langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mabawa yake. Nanyi mtatoka nje na kurukaruka kama ndama aliyeachiwa kutoka zizini. 3Kisha ninyi mtawakanyaga waovu, nao watakuwa majivu chini ya nyayo za miguu yenu siku ile nitakayofanya mambo haya,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote. 4“Kumbukeni sheria ya mtumishi wangu Mose, amri na sheria nilizompa huko Horebu kwa ajili ya Israeli wote. 5“Tazama, nitawapelekea nabii Eliya kabla ya kuja siku ile iliyo kuu na ya kutisha ya Bwana. 6Ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, la sivyo nitakuja na kuipiga nchi kwa laana.”

Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.

Urahisi wa kusoma

Chagua kinachokusaidia. Chaguo lako linahifadhiwa kwenye kifaa hiki.

Ukubwa wa maandishi

Unapendelea mipangilio ya kifaa chako mwenyewe (kukuza, kisoma skrini, hali ya giza)? Inafanya kazi hapa pia.