1Mzee: Kwa Gayo rafiki yangu, nimpendaye katika kweli. 2Mpendwa, naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya njema kama vile roho yako ifanikiwavyo. 3Ilinifurahisha sana baadhi ya ndugu walipokuja na kutueleza juu ya uaminifu wako katika kweli na jinsi unavyoendelea kuenenda katika hiyo kweli. 4Sina furaha kubwa kuliko hii, kusikia kwamba watoto wangu wanaenenda katika kweli. 5Rafiki mpendwa, wewe ni mwaminifu kwa yale unayowatendea ndugu, ingawa wao ni wageni kwako. 6Wameshuhudia kuhusu upendo wako mbele ya kanisa. Utafanya vyema ukiwasafirisha kama inavyostahili kwa Mungu. 7Ilikuwa ni kwa ajili ya hilo Jina waliondoka, bila kukubali kupokea msaada wowote kutoka kwa watu wasioamini. 8Kwa hiyo imetupasa sisi kuonyesha ukarimu kwa watu kama hao ili tuweze kutenda kazi pamoja kwa ajili ya kweli. 9Nililiandikia kanisa, lakini Deotrefe, yeye apendaye kujifanya wa kwanza, hakubali mamlaka yetu. 10Hivyo kama nikija, nitakumbuka matendo yake atendayo, akitusingizia kwa maneno ya hila. Wala hatosheki na hayo anayotusingizia, bali pia hukataa kuwakaribisha ndugu, na hata huwazuia wale walio tayari kufanya hivyo na kuwafukuza watoke kanisani. 11Rafiki mpendwa, usiige lile lililo baya bali lile lililo jema. Yeyote atendaye mema atoka kwa Mungu, bali atendaye mabaya hajamwona Mungu. 12Kila mtu ameshuhudia mema kuhusu Demetrio, vivyo hivyo hata na hiyo kweli yenyewe. Sisi pia twashuhudia mema juu yake, nanyi mwajua kwamba ushuhuda wetu ni kweli. 13Ninayo mambo mengi ya kukuandikia, lakini sipendi kuandika kwa kalamu na wino. 14Badala yake, nataraji kukuona upesi, nasi tutaongea pamoja ana kwa ana. 15Amani iwe kwako. Rafiki zetu walioko hapa wanakusalimu. Wasalimu hao rafiki zetu walioko huko, kila mmoja kwa jina lake.
1The elder to Gaius the beloved, whom I love in truth. 2Beloved, I pray that you may prosper in all things and be healthy, even as your soul prospers. 3For I rejoiced greatly, when brothers came and testified about your truth, even as you walk in truth. 4I have no greater joy than this, to hear about my children walking in truth. 5Beloved, you do a faithful work in whatever you accomplish for those who are brothers and strangers. 6They have testified about your love before the assembly. You will do well to send them forward on their journey in a way worthy of God, 7because for the sake of the Name they went out, taking nothing from the Gentiles. 8We therefore ought to receive such, that we may be fellow workers for the truth. 9I wrote to the assembly, but Diotrephes, who loves to be first among them, doesn’t accept what we say. 10Therefore if I come, I will call attention to his deeds which he does, unjustly accusing us with wicked words. Not content with this, neither does he himself receive the brothers, and those who would, he forbids and throws out of the assembly. 11Beloved, don’t imitate that which is evil, but that which is good. He who does good is of God. He who does evil hasn’t seen God. 12Demetrius has the testimony of all, and of the truth itself; yes, we also testify, and you know that our testimony is true. 13I had many things to write to you, but I am unwilling to write to you with ink and pen; 14but I hope to see you soon, and we will speak face to face. Peace be to you. The friends greet you. Greet the friends by name.
1De ouderling aan den geliefden Gajus, welken ik in waarheid liefheb. 2Geliefde, voor alle dingen wens ik, dat gij welvaart en gezond zijt, gelijk uw ziel welvaart. 3Want ik ben zeer verblijd geweest, als de broeders kwamen, en getuigden van uw waarheid, gelijk gij in de waarheid wandelt. 4Ik heb geen meerdere blijdschap dan hierin, dat ik hoor, dat mijn kinderen in de waarheid wandelen. 5Geliefde, gij doet trouwelijk, in al hetgeen gij doet aan de broederen en aan de vreemdelingen, 6Die getuigd hebben van uw liefde, in de tegenwoordigheid der Gemeente; welken indien gij geleide doet, gelijk het Gode waardig is, zo zult gij weldoen. 7Want zij zijn voor Zijn Naam uitgegaan, niets nemende van de heidenen. 8Wij dan zijn schuldig de zodanigen te ontvangen, opdat wij medearbeiders mogen worden der waarheid. 9Ik heb aan de Gemeente geschreven; maar Diotrefes, die onder hen zoekt de eerste te zijn, neemt ons niet aan. 10Daarom, indien ik kom, zo zal ik in gedachtenis brengen zijn werken, die hij doet, met boze woorden snaterende tegen ons; en hiermede niet vergenoegd zijnde, zo ontvangt hij zelf de broeders niet, en verhindert degenen, die het willen doen, en werpt ze uit de Gemeente. 11Geliefde, volgt het kwade niet na, maar het goede. Die goed doet, is uit God; maar die kwaad doet, heeft God niet gezien. 12Aan Demetrius wordt getuigenis gegeven van allen, en van de waarheid zelve; en wij getuigen ook, en gij weet, dat onze getuigenis waarachtig is. 13Ik had veel te schrijven, maar ik wil u niet schrijven met inkt en pen; 14Maar ik hoop u haast te zien, en wij zullen mond tot mond spreken. Vrede zij u. De vrienden groeten u. Groet de vrienden met name.
Bonyeza Enter ili kuuwekea mstari huu rangi, kuandika maelezo au kuunakili. Vitufe vya mishale vinakupeleka kwenye mstari unaofuata.
Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.