1Hatimaye, ndugu, tuombeeni ili Neno la Bwana lipate kuenea kwa haraka na kuheshimiwa kila mahali, kama vile ilivyokuwa kwenu. 2Ombeni pia ili tupate kuokolewa kutokana na watu waovu na wabaya, kwa maana si wote wanaoamini. 3Lakini Bwana ni mwaminifu, naye atawaimarisha ninyi na kuwalinda kutokana na yule mwovu. 4Nasi tuna tumaini katika Bwana ya kuwa mnafanya na mtaendelea kufanya yale tuliyowaagiza. 5Bwana aiongoze mioyo yenu katika upendo wa Mungu na katika saburi ya Kristo. 6Ndugu, tunawaagiza katika Jina la Bwana Yesu Kristo, jitengeni na kila ndugu ambaye ni mvivu na ambaye haishi kufuatana na maagizo tuliyowapa. 7Maana ninyi wenyewe mnajua jinsi iwapasavyo kufuata mfano wetu. Sisi hatukuwa wavivu tulipokuwa pamoja nanyi, 8wala hatukula chakula cha mtu yeyote pasipo kukilipia. Badala yake tulifanya kazi kwa bidii usiku na mchana, ili tusimlemee mtu yeyote miongoni mwenu. 9Tulifanya hivi, si kwa sababu hatukuwa na haki ya kupata msaada kama huo, bali ndio sisi wenyewe tuwe kielelezo. 10Kwa maana hata tulipokuwa pamoja nanyi, tuliwapa amri kwamba: “Mtu yeyote asiyetaka kufanya kazi, hata kula asile.” 11Kwa kuwa tunasikia kwamba baadhi ya watu miongoni mwenu ni wavivu. Hawafanyi kazi bali hujishughulisha na mambo ya wengine. 12Basi watu kama hao tunawaagiza na kuwahimiza katika Bwana Yesu Kristo, kwamba wafanye kazi kwa utulivu kwa ajili ya chakula chao wenyewe. 13Kwa upande wenu, ndugu, ninyi kamwe msichoke katika kutenda mema. 14Ikiwa mtu yeyote hayatii maagizo yetu yaliyoko katika barua hii, mwangalieni sana mtu huyo. Msishirikiane naye, ili apate kuona aibu. 15Lakini msimhesabu kuwa adui, bali mwonyeni kama ndugu. 16Basi, Bwana wa amani mwenyewe awapeni amani nyakati zote na kwa kila njia. Bwana awe nanyi nyote. 17Mimi, Paulo, ninaandika salamu hizi kwa mkono wangu mwenyewe. Hii ndio alama ya utambulisho katika barua zangu zote. Hivi ndivyo niandikavyo. 18Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi nyote. Amen.
1Finally, brothers, pray for us, that the word of the Lord may spread rapidly and be glorified, even as also with you; 2and that we may be delivered from unreasonable and evil men; for not all have faith. 3But the Lord is faithful, who will establish you, and guard you from the evil one. 4We have confidence in the Lord concerning you, that you both do and will do the things we command. 5May the Lord direct your hearts into the love of God, and into the patience of Christ. 6Now we command you, brothers, in the name of our Lord Jesus Christ, that you withdraw yourselves from every brother who walks in rebellion, and not after the tradition which they received from us. 7For you know how you ought to imitate us. For we didn’t behave ourselves rebelliously among you, 8neither did we eat bread from anyone’s hand without paying for it, but in labor and travail worked night and day, that we might not burden any of you; 9not because we don’t have the right, but to make ourselves an example to you, that you should imitate us. 10For even when we were with you, we commanded you this: “If anyone will not work, neither let him eat.” 11For we hear of some who walk among you in rebellion, who don’t work at all, but are busybodies. 12Now those who are that way, we command and exhort in the Lord Jesus Christ, that with quietness they work, and eat their own bread. 13But you, brothers, don’t be weary in doing well. 14If any man doesn’t obey our word in this letter, note that man, that you have no company with him, to the end that he may be ashamed. 15Don’t count him as an enemy, but admonish him as a brother. 16Now may the Lord of peace himself give you peace at all times in all ways. The Lord be with you all. 17The greeting of me, Paul, with my own hand, which is the sign in every letter: this is how I write. 18The grace of our Lord Jesus Christ be with you all. Amen.
1Voorts, broeders, bidt voor ons, opdat het Woord des Heeren zijn loop hebbe, en verheerlijkt worde, gelijk ook bij u; 2En opdat wij mogen verlost worden van de ongeschikte en boze mensen; want het geloof is niet aller. 3Maar de Heere is getrouw, Die u zal versterken en bewaren van den boze. 4En wij vertrouwen van u in den Heere, dat gij, hetgeen wij u bevelen, ook doet, en doen zult. 5Doch de Heere richte uw harten tot de liefde van God, en tot de lijdzaamheid van Christus. 6En wij bevelen u, broeders, in den Naam van onzen Heere Jezus Christus, dat gij u onttrekt van een iegelijk broeder, die ongeregeld wandelt, en niet naar de inzetting, die hij van ons ontvangen heeft. 7Want gijzelven weet, hoe men ons behoort na te volgen; want wij hebben ons niet ongeregeld gedragen onder u; 8En wij hebben geen brood bij iemand gegeten voor niet, maar in arbeid en moeite, nacht en dag werkende, opdat wij niet iemand van u zouden lastig zijn; 9Niet, dat wij de macht niet hebben, maar opdat wij onszelven u geven zouden tot een voorbeeld, om ons na te volgen. 10Want ook toen wij bij u waren, hebben wij u dit bevolen, dat, zo iemand niet wil werken, hij ook niet ete. 11Want wij horen, dat sommigen onder u ongeregeld wandelen, niet werkende, maar ijdele dingen doende. 12Doch de zodanigen bevelen en vermanen wij door onzen Heere Jezus Christus, dat zij met stilheid werkende, hun eigen brood eten. 13En gij, broeders, vertraagt niet in goed te doen. 14Maar indien iemand ons woord, door deze brief geschreven, niet gehoorzaam is, tekent dien; en vermengt u niet met hem, opdat hij beschaamd worde; 15En houdt hem niet als een vijand, maar vermaant hem als een broeder. 16De Heere nu des vredes Zelf geve u vrede te allen tijd, in allerlei wijze. De Heere zij met u allen. 17De groetenis met mijn hand, van Paulus; hetwelk is een teken in iederen zendbrief; alzo schrijf ik. 18De genade van onzen Heere Jezus Christus zij met u allen. Amen.
Bonyeza Enter ili kuuwekea mstari huu rangi, kuandika maelezo au kuunakili. Vitufe vya mishale vinakupeleka kwenye mstari unaofuata.
Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.